Orodha ya Hadithi

Mwenye kwenda mbio kuwasaidia wajane na masikini, ni kama mwenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Msizifanye nyumba zenu kuwa makaburi, na wala msilifanye kaburi langu kuwa sikukuu, na mniombee rehema juu yangu, kwani maombi yenu hunifikia mahala popote mtakapokuwa.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Swala tano, na Ijumaa mpaka Ijumaa, na ramadhani mpaka ramadhani vinafuta madhambi yaliyo kati yake, yatakapoepukwa madhambi makubwa.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika halali iko wazi na hakika haramu iko wazi, na kati ya hayo kuna mambo yenye kutatiza hawayafahamu wengi katika watu, atakaye yaepuka mambo yenye kutatiza basi atakuwa ameitakasa dini yake na heshima yake, na atakayetumbukia katika mambo yenye kutatiza atakuwa katumbukia katika haramu.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Laiti nyinyi mgetegemea kwa Mwenyezi Mungu ukweli wa kumtegemea, basi angekuruzukuni kama anavyowaruzuku ndege, wanatoka asubuhi wakiwa na njaa, wanarudi jioni wakiwa wameshiba
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Ametenda dhambi mja, akasema: Ewe Mola wangu nisamehe mimi dhambi langu, akasema Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka: Mja wangu katenda dhambi, na akajua kuwa ana Mola anayesamehe dhambi, na analichukua dhambi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Kila wema ni sadaka
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Haingii peponi mkataji (udugu)
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayependa kukunjuliwa katika riziki yake, na kucheleweshwa katika ajali yake basi naaunge udugu wake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika dua ndiyo ibada
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakuna kitu kitukufu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko dua
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayesema: Sub-haana llaahi wabihamdihi- Ametakasika Mwenyezi Mungu na sifa njema ni zake- kwa siku mara mia moja, atasamehewa makosa yake hata kama yatakuwa mfano wa povu la bahari
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Mwenye kumtakia Mwenyezi Mungu kheri kwake humpa ufahamu katika dini
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu basi atapata jema moja na jema hilo kwa mema kumi mfano wake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakuna mja yeyote atakayeshuhudia kuwa hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammdi ni mja wake kwa kusadikisha kutoka moyoni mwake ispokuwa atamharamisha Mwenyezi Mungu kuingia motoni.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Alitoka Muawiya- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akakuta duara msikitini, akasema: Nini kimewakalisheni? wakasema: tumekaa tunamtaja Mwenyezi Mungu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Mchungeni(mfuatilieni) Muhammadi -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa watu wa nyumba yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
"Haya (Aibu) haiji ila kwa kheri"
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hana mja wangu muumini toka kwangu malipo yoyote pindi ninapomchukua kipenzi chake katika familia yake duniani kisha akasubiri (malipo mazuri) zaidi ya pepo
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hebu rudi kwa wazazi wako, na ukaishi nao vizuri
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Dinari bora anayoitoa mtu: ni Dinari anayoitoa kwa familia yake, na Dinari anayoitoa kwa mnyama wake katika njia ya Mwenyezi Mungu, na Dinari anayoitoa kwa jamaa zake katika njia ya Mwenyezi Mungu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Msilifanye kaburi langu kuwa sikukuu, wala nyumba zenu kuwa makaburi, na nitakieni rehma, kwani dua zenu hunifikia popote mlipo
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayewalea mabinti wawili mpaka wakafikia utu uzima atakuja siku ya kiyama mimi na yeye ni kama vidole hivi viwili
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, Hamtoingia peponi mpaka muamini, na hamtoamini mpaka mpendane, je nisikufahamisheni juu ya jambo ambalo mkilifanya mtapendana? toleaneni salamu kwa wingi kati yenu.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nilimuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ni amali ipi inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu? Akasema: Ni (kuiswali) swala kwa wakati wake. Nikasema: kisha nini? Akasema: Ni kuwatendea wema wazazi wawili
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Mikosi ya ndege ni shirki, na hakuna yeyote miongoni mwetu ispokuwa (ana chembe ya hilo), lakini Mwenyezi Mungu huliondoa kwa kumtegemea
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nitampa bendera kesho mtu ambaye anampenda Allah na Mtume wake,na anapendwa na Allah na Mtume wake,kupitia yeye Allah ataleta ushindi.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hivi hukujua kuwa uislamu hufuta madhambi yaliyokuwa kabla yake, na kuwa kuhama kunafuta madhambi yaliyokuwa kabla yake, nakuwa Hija inafuta madhambi yaliyokuwa kabla yake?
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Mcheni Mwenyezi Mungu na mswali swala zenu tano, na mfunge mwezi wenu, na mtekeleze zaka za mali zenu, na muwatii viongozi wenu, mtaingia pepo ya Mola wenu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Je! nikujulisheni mambo ambayo yakifanyika Allah hufuta madhambi na hupandisha daraja kwa mambo hayo? wakasema: ndiyo, Ewe Mtume wa Allah, akasema: Kutawadha vizuri wakati wa baridi, na kuzidisha hatua kwenda msikitini, na kusubiria swala baada ya swala huko ndiko kuizuia nafsi katika mambo ya kheri.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Je nikujulisheni matendo yenu bora, na matukufu mbele ya mfalme wenu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Ameangukia pua (kapata hasara), kisha Ameangukia pua (kapata hasara), kisha Ameangukia pua (kapata hasara), atakayewapata wazazi wake wawili wakati wa ukubwa mmoja wao au wote wawili na akawa hakuingia peponi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Wametangulia watu wa kipekee
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nilikutana na Ibrahimu usiku niliochukuliwa, Akasema: Ewe Muhammadi wafikishie umma wako salamu zangu, na uwaeleze kuwa pepo ina udongo mzuri, ina maji matam, nakuwa imenyooka na kulingana sawa, nakuwa mimea yake: ni (kusema) Sub-haana llaah -Ametakasika Mwenyezi Mungu, Na Alhamdulillaah -Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu, Na Laa ilaaha illa llaah -Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na Allaahu Akbar -Mwenyezi Mungu Mkubwa.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Ikiwa kama utakuwa kama ulivyosema, basi ni kana kwamba unawalisha majivu ya moto (dhambi wanazozipata ni kama mtu anayekula majivu ya moto), Na bado anaendelea kuwa pamoja nawe msaidizi kutoka kwa Mwenyezi Mungu dhidi yao, madam bado uko katika hali hiyo
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakuna watu wowote watasimama katika kikao ambacho hawamtaji Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake, isipokuwa watanyanyuka mithili ya mzoga wa punda, na wanakua na majuto
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hainifurahishi mimi kumiliki dhahabu mfano wa mlima huu wa Uhudi, zikapita siku tatu nikawa hata na dinari moja (katika mali hiyo) isipokuwa kiasi ninachokihifadhi kwaajili ya kulipa deni, isipokuwa niseme kwa waja wa Mwenyezi Mungu hivi na vile.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani mwenye haki zaidi ya kumfanyia wema wa karibu? akasema: mama yako, kisha mama yako kisha mama yako, kisha baba yako, kisha anayefuata kwa ukaribu kisha nayemfuata kwa ukaribu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa