+ -

عَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، قَالَ: لَأُحَدِّثَنَّكُمْ حَدِيثًا سَمِعْتُهُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لاَ يُحَدِّثُكُمْ بِهِ أَحَدٌ غَيْرِي: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«إِنَّ مِنْ أَشْرَاطِ السَّاعَةِ أَنْ يُرْفَعَ العِلْمُ، وَيَكْثُرَ الجَهْلُ، وَيَكْثُرَ الزِّنَا، وَيَكْثُرَ شُرْبُ الخَمْرِ، وَيَقِلَّ الرِّجَالُ، وَيَكْثُرَ النِّسَاءُ حَتَّى يَكُونَ لِخَمْسِينَ امْرَأَةً القَيِّمُ الوَاحِدُ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 5231]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema: Nitawahadithieni Hadithi nimeisikia kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-, na hadithi hiyo hatowahadithia yeyote asiyekuwa mimi: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake anasema:
"Kwa hakika miongoni mwa alama za Kiyama ni kuondolewa elimu, na kuzidi ujinga, na kukithiri uzinifu, unywaji pombe, na wanaume watakuwa wachache na wanawake watakuwa wengi mpaka itafikia wanawake hamsini kusimamiwa na mwanaume mmoja."

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 5231]

Ufafanuzi

Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa katika alama za kukaribia Kiyama ni kuondolewa elimu ya sheria na kuondolewa kwake itakuwa ni kwa kufa wanachuoni. Na matokeo yake utazidi na utaenea ujinga, na uzinifu utaenea na uchafu, na unywaji pombe utazidi na idadi ya wanaume itapungua na ya wanawake itazidi; Mpaka itafikia hatua mwanaume mmoja atabeba mambo yao na kusimamia maslahi yao.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف البلغارية Luqadda Asariga اليونانية الأوزبكية الأوكرانية الجورجية اللينجالا المقدونية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumewekwa wazi baadhi ya alama za Kiyama.
  2. Kujua muda wa Kiyama ni katika mambo ya ghaibu (yasiyoonekana wala kujulikana) ni katika mambo ambayo Mwenyezi Mungu ameyaficha.
  3. Himizo juu ya kujifunza elimu ya kisheria kabla ya kukosekana kwake.