عن خَولة الأنصاريةِ رضي الله عنها قالت: سمعت النبي صلى الله عليه وسلم يقول:
«إِنَّ رِجَالًا يَتَخَوَّضُونَ فِي مَالِ اللهِ بِغَيْرِ حَقٍّ، فَلَهُمُ النَّارُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 3118]
المزيــد ...
Kutoka kwa Khaula Al-Answariya -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Hakika watu wanaotumia mali ya Mwenyezi Mungu pasina haki, hao (wana adhabu ya) moto siku ya Kiyama".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 3118]
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu watu wanaotumia mali ya waislamu kwa batili, na wanaichukua pasina haki, na maana hii inajumuisha kuanzia ukusanyaji wake, na uchumaji wake bila uhalali wake, na utoaji wake katika sehemu zisizo sahihi, na inaingia katika hilo kula mali ya yatima na mali ya wakfu, na kutotunza amana, na kuchukua chochote katika mali ya umma bila ya haki.
Ameeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa malipo yao ni moto siku ya Kiyama.