عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ:
«إِيَّاكُمْ وَالظَّنَّ؛ فَإِنَّ الظَّنَّ أَكْذَبُ الْحَدِيثِ، وَلَا تَحَسَّسُوا، وَلَا تَجَسَّسُوا، وَلَا تَحَاسَدُوا، وَلَا تَدَابَرُوا، وَلَا تَبَاغَضُوا، وَكُونُوا عِبَادَ اللهِ إِخْوَانًا».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 6064]
المزيــد ...
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Tahadharini na dhana; kwani dhana ni mazungumzo ya uongo mno, na wala msitiliane shaka (kwa kuhisiana vibaya), na wala msichunguzane, na wala msihusudiane, na wala msitengane, na wala msichukiane, na kuweni waja wa Mwenyezi Mungu ndugu wamoja"
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 6064]
Anakataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na anatahadharisha baadhi ya yale yanayoweza kupelekea kufarakana na uadui baina ya waislamu, na miongoni mwayo:
(Dhana) Nazo ni tuhuma zinazojitokeza ndani ya moyo pasina ushahidi, na akabainisha kuwa hayo ni mazungumzo ya uongo mno.
Na kuhusu (kuhisiana vibaya): Nako ni kutafuta aibu za watu kwa kutazama au kusikiliza.
(Na kupelelezana): Nako ni kutafuta yaliyofichikana miongoni mwa mambo, na hii hutumika zaidi katika shari.
Na kuhusu: (Husuda) nako ni kuchukia kupatikana kwa neema kwa watu wengine.
Na kuhusu (Kutengana) kwa kuwapuuza baadhi ya watu wenzao, hamsalimii wala hamtembelei ndugu yake muislamu,
Na kuhusu: (Kuchukiana) na kuchukia na kubeza, kama kuwaudhi watu wengine, na kutotabasamu, na kukutana nao kwa sura mbaya.
Kisha akazungumza neno moja linalokusanya kila kitu, ambalo litatengeneza hali za waislamu baadhi yao kwa baadhi: (Na kuweni waja wa Mwenyezi Mungu ndugu wamoja). Udugu ni kiunganishi kinachounganisha mahusiano kati ya watu, na kinazidisha mapenzi na kuzoeana baina yao.