عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«سِبَابُ المُسْلِمِ فُسُوقٌ، وَقِتَالُهُ كُفْرٌ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 48]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Kumtukana Muislamu ni ufasiki (kutoka nje ya mipaka), na kupigana naye ni ukafiri."
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 48]
Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemkataza muislamu kumshutumu na kumtukana ndugu yake muislamu, nakuwa hilo ni katika ufasiki ambao ni kutoka nje ya utiifu wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, nakuwa muislamu kukabiliana na ndugu yake muislamu ni katika matendo ya ukafiri, lakini ni ukafiri mdogo.