عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعاً: "اجتنبوا السبع المُوبِقَات، قالوا: يا رسول الله، وما هُنَّ؟ قال: الشركُ بالله، والسحرُ، وقَتْلُ النفسِ التي حَرَّمَ الله إلا بالحق، وأكلُ الرِّبا، وأكلُ مالِ اليتيم، والتَّوَلّي يومَ الزَّحْفِ، وقذفُ المحصناتِ الغَافِلات المؤمنات".
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Jiepusheni na mambo saba yenye kuangamiza, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni yapi hayo? Akasema: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na uchawi, na kuuwa nafsi aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu ispokuwa kwa haki, na kula riba, na kula mali ya yatima, na kukimbia siku ya mapambano, na kuwazulia machafu wanawake waumini wenye kujihifadhi wenye kujizuia na machafu".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Anauamrisha rehema na Amani ziwe juu yake umma wake kujiweka mbali na makosa saba yenye kuangamiza, na alipoulizwa kuhusu makosa hayo ni yapi? Akayabainisha kuwa ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, kwa kumuwekea washirika kwa namna yoyote ile itakayokuwa, na kaanza na ushirikina kwasababu hilo ndio kubwa la madhambi, na kuuwa nafsi ambayo amekataza Mwenyezi Mungu kuiuwa ispokuwa kwa kigezo cha kisheria, na uchawi, na kutumia riba kwa kula au kwa lolote katika namna za kunufaika, na kufanya dhulma katika mali za mtoto ambaye baba yake amekufa, na kukimbia katika vita pamoja na makafiri, na kuwatuhumu wanawake huru waliojihifadhi kwa zinaa.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese German Kijapani Pashto Kiassam Albanian
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kuharamishwa shirki, nakuwa yenyewe ni kosa kubwa na ni dhambi kubwa.
  2. Kuharamishwa uchawi, nakuwa ni katika makosa makubwa yenye kuangamiza, na ni katika vitenguzi vya uislamu.
  3. Kuharamishwa kuuwa nafsi bila hatia.
  4. Kufaa kuuwa nafsi ikiwa kuna haki kama kisasi na kuritadi (kutoka katika uislamu) na kufanya zinaa baada ya kuoa au kuolewa.
  5. Uharamu wa riba na ukubwa wa hatari yake.
  6. Uharamu wa kufanya uadui na dhulma katika mali ya yatima.
  7. Uharamu wa kukimbia vitani.
  8. Uharamu wa kutupia (kusingizia) zinaa au ulawiti.
  9. Nikuwa kumsingizia kafiri si katika madhambi makubwa.