عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه مرفوعاً: "ألا أخبركم بما هو أَخْوَفُ عليكم عندي من المسيح الدجال؟ قالوا: بلى يا رسول الله، قال: الشرك الخفي يقوم الرجل فيصلي فَيُزَيِّنُ صلاته لما يرَى من نَظَرِ رَجُلٍ".
[حسن] - [رواه ابن ماجه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Saidi Al Khudriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Je nisikuelezeni kwa kile ambacho ninakiogopea zaidi kwenu nyinyi kuliko hata masihi dajali? Wakasema: Tueleze ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema: Ni shirki iliyofichikana, anasimama mtu kuswali anapendezesha swala yake kwakuwa anaona kuna mtu anamtazama".
Ni nzuri - Imepokelewa na Ibnu Maajah

Ufafanuzi

Walikuwa maswahaba wakikumbushana fitina ya masihi dajali na wakiogopeshana juu yake, akawaeleza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa kuna jambo la haramu analowaogopea kuliko hata hofu ya fitina ya masihi dajali, nayo ni shirki katika nia na makusudio ambayo haionekani kwa watu, kisha akalifasiri hilo kwa kuyafanya vizuri matendo ambayo hutafutiwa kwayo radhi za Mwenyezi Mungu kwaajili ya kuwaonyesha watu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kireno
Kuonyesha Tarjama