عن عمر بن الخطاب رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
«إِنَّمَا الْأَعْمَالُ بِالنِّيَّةِ، وَإِنَّمَا لِامْرِئٍ مَا نَوَى، فَمَنْ كَانَتْ هِجْرَتُهُ إِلَى اللهِ وَرَسُولِهِ، فَهِجْرَتُهُ إِلَى اللهِ وَرَسُولِهِ، وَمَنْ كَانَتْ هِجْرَتُهُ لِدُنْيَا يُصِيبُهَا أَوِ امْرَأَةٍ يَتَزَوَّجُهَا، فَهِجْرَتُهُ إِلَى مَا هَاجَرَ إِلَيْهِ».
وفي لفظ للبخاري: «إِنَّمَا الْأَعْمَالُ بِالنِّيَّاتِ، وَإِنَّمَا لِكُلِّ امْرِئٍ مَا نَوَى».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 1907]
المزيــد ...
Imepokewa kutoka kwa Omar Bin Khattwab- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-
"Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu hulipwa kwa lile alilonuia, atakayekuwa kuhama kwake ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, (basi malipo yake yatakuwa) ni kuhama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na atakayekuwa kuhama kwake ni kwa ajili ya kuipata dunia, au kwa ajili ya mwanamke atakaemuoa, basi kuhama kwake kutakuwa ni kwa kile alichokiendea." Na lafudhi ya Bukhari: ""Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu hulipwa kwa lile alilonuia."
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 1907]
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa matendo yote huzingatiwa nia, na hukumu hii ni ya ujumla katika amali zote, kwanzia ibada na miamala, atakaye kusudia kupata masilahi katika amali yake hatopata zaidi ya masilahi na wala hatopata thawabu, na atakayekusudia katika amali yake kujiweka karibu na Allah Mtukufu, atapata thawabu na malipo kupitia amali yake hata kama litakuwa ni jambo la kawaida, kama kula na kunywa.
Kisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akapiga mfano wa kuweka wazi namna gani nia inaathiri matendo pamoja nakuwa huonekana yote yako sawa katika muonekano wa juu, akaweka wazi kuwa atakayekusudia katika kuhama kwake na kuacha nchi yake ni kutafuta radhi za Mola wake, basi kuhama kwake kutakuwa ni kwa kisheria na kunakubalika, atalipwa kwa sababu ya ukweli wa nia yake, na atakayekusudia kwa kuhama kwake ni kupata masilahi ya kidunia, kama mali, au cheo, au mke, basi hatopata kwa kuhama kwake huko zaidi ya manufaa aliyoyakusudia, na wala hatokuwa na fungu la malipo na thawabu.