عَنْ أَبي مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«إِنَّ مِمَّا أَدْرَكَ النَّاسُ مِنْ كَلاَمِ النُّبُوَّةِ الأُولَى: إِذَا لَمْ تَسْتَحْيِ فَاصْنَعْ مَا شِئْتَ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 6120]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Hakika katika yale waliyoyakuta watu miongoni mwa maneno ya kiutume ya mwanzo, usipokuwa na haya basi fanya ulitakalo".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 6120]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa katika yale yaliyokuja na usia ndani yake kutoka kwa Manabii waliotangulia, na yakaenea kwa watu na watu wakarithishana kutoka kwao karne baada ya karne, mpaka yakamfikia wa mwanzo katika umma huu, ni; tazama unayotaka kuyafanya, ikiwa yatakuwa ni katika mambo ambayo si aibu basi fanya, na ikiwa ni katika mambo ya aibu basi acha; kwa sababu kinachozuia kufanya matendo mabaya ni haya, atakayekosa aibu basi hutumbukia katika kila machafu na maovu.