+ -

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال:
«كان رجلٌ يُدَايِنُ الناسَ، فكان يقول لفتاه: إذا أتيتَ مُعسِرًا فتجاوز عنه، لعل اللهَ يَتجاوزُ عنا، فلقي اللهَ فتجاوز عنه».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 1562]
المزيــد ...

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Kulikuwa na mtu akiwakopesha watu,basi alikuwa akisema kumwambia kijana wake (Akienda kudai): Ukifika kwa mwenye hali ngumu, basi msamehe, huenda nasi Allah akatusamehe (alipokufa) akakutana na Allah, akamsamehe".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 1562]

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kuhusu bwana mmoja aliyekuwa akiamiliana na watu kwa mkopo, au akiwauzia kwa mkopo, Na alikuwa akisema kumwambia kijana wake aliyekuwa akikusanya madeni yaliyoko kwa watu: Utakapomwendea mdaiwa na akawa hana cha kulipa deni analodaiwa kwa sababu ya kushindwa "Basi, msamehe"; Ima kwa kumpa muda zaidi na kutong'ang'ania kumdai, Au kwa kukubali alichonacho hata kama kina mapungufu, na hiyo ni kwa hamu yake na tamaa yake ya kutaka Allah asimuadhibu na amsamehe, Alipofariki Allah akamsamehe na hakumuadhibu kwa makosa yake mengine.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف البلغارية Luqadda Asariga الأكانية الأوزبكية الأوكرانية الجورجية اللينجالا المقدونية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Wema katika kuamiliana na watu na kuwasamehe na kumpa uhuru mwenye hali ngumu ni katika sababu kubwa za mja kusalimika siku ya Kiyama.
  2. Kuwafanyia wema viumbe na kutakasa matendo kwa ajili ya Allah na kutaraji katika rehema zake ni katika sababu za kupata msamha wa madhambi.