عن أبي هريرة رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «الصلوات الخمس، والجمعة إلى الجمعة، ورمضان إلى رمضان مُكَفِّراتٌ لما بينهنَّ إذا اجتُنبَت الكبائر».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Kutoka kwa Mtume rehema na Amani zimfikie, Amesema: "Swala tano, na Ijumaa mpaka Ijumaa, na ramadhani mpaka ramadhani vinafuta madhambi yaliyo kati yake, yatakapoepukwa madhambi makubwa".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Swala tano zinafuta yaliyo kati yake katika madhambi- nayo ni yale madogo- ispokuwa madhambi makubwa hakuna kinachoyafuta ispokuwa toba, na hivyo hivyo Ijumaa mpaka ijumaa inayofuata, na hivyo hivyo funga ya Ramadhani mpaka Ramadhani iliyo baada yake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese German Kijapani Pashto Kiassam Albanian
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Nikuwa kutekeleza wajibu huu kwa namna nzuri inakuwa ni sababu ya kuyasamehe Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka kwa fadhila zake na rehema zake yale yaliyojitokeza kati yake miongoni mwa madhambi madogo.
  2. Kugawanyika kwa madhambi katika madhambi madogo na makubwa.