عن أنس بن مالك رضي الله عنه قال سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «من أحبّ أن يُبْسَطَ عليه في رزقه، وأن يُنْسَأَ له في أَثَرِهِ؛ فَلْيَصِلْ رحمه».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Anas bin Maliki Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Amesema: Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake akisema: "Atakayependa kukunjuliwa katika riziki yake, na kucheleweshwa katika ajali yake basi naaunge udugu wake".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Katika hadithi hii kuna himizo la kuunga udugu, na kubainishwa baadhi ya faida zake, pamoja na hilo ni kuhakikisha kupata radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu-, kwani hilo ni sababu pia ya kupata thawabu za haraka kwa kuyapata mambo yanayopendeka zaidi kwa mja, nakuwa ni sababu ya kukunjuliwa riziki yake na ni sababu ya kurefushwa umri. Na kauli yake Mtukufu: "Na haicheleweshi Mwenyezi Mungu nafsi yoyote muda wake unapofikia" Maana yake ni muda wake ambao itaufikia baada ya kufanya kwake sababu za kurefushwa umri, tukichukulia kwa mfano umri wa mtu ni miaka hamsini, nakuwa yeye kabla ya kufa ataunga udugu na ukawa umri wake ni miaka sitini, basi hautocheleweshwa zaidi ya sitini, na hayo yote Mwenyezi Mungu Mtukufu anayajua tangu mwanzo, lakini linaweza kufichikana hilo kwa baadhi ya Malaika, Na kauli yake Mtukufu-: "Anayafuta Mwenyezi Mungu ayatakayo na anathibitisha" Yaani katika kurasa za Malaika "Na kwake kuna mama wa kitabu" ambacho kumeandikwa ndani yake ufafanuzi wa kila kitu, hakibadiliki ndani yake chochote.

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kichina Kifursi Kihindi Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese German Kijapani
Kuonyesha Tarjama

Faida nyingi

  1. Kuhimizwa na kupupia juu ya kuunga udugu.
  2. Kuunga udugu ni sababu ya nguvu aliyoiweka Mwenyezi Mungu katika kukunjua riziki ya muungaji na kurefuka kwa umri wake.
  3. Malipo huendana na aina ya matendo, atakayeunga udugu wake kwa wema na ih-sani, Mwenyezi Mungu atamuunga katika umri wake na riziki yake.
  4. Kuthibitishwa sababu; kwasababu Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- kathibitisha sababu- Nayo ni: -kurefushwa umri na kukunjuliwa katika riziki-.