عن أبي صِرْمة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال:
«مَنْ ضَارَّ ضَارَّ اللهُ بِهِ، وَمَنْ شَاقَّ شَقَّ اللهُ عَلَيْهِ».

[حسن] - [رواه أبو داود والترمذي وابن ماجه وأحمد] - [سنن الترمذي: 1940]
المزيــد ...

kutoka kwa Abuu Swirma -Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Atakayedhuru Mwenyezi Mungu naye atamdhuru, na atakayewatia watu ugumu Mwenyezi Mungu naye atamtilia ugumu".

[Ni nzuri (Hasan)] - [Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad] - [Sunanu Tirmidhiy - 1940]

Ufafanuzi

Ametahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutomuingizia madhara muislamu, au kumtia tabu katika jambo lolote katika mambo yake; Yeye mwenyewe au mali yake au familia yake, nakuwa atakayefanya hivyo basi Mwenyezi Mungu atamlipa na atamuadhibu kwa jinsi alivyomfanyia mwenzake.

Katika Faida za Hadithi

  1. Uharamu wa kumdhuru muislamu na kumtia tabu.
  2. Allah huwalipizia kisasi waja wake.
Kuonyesha Tarjama
Lugha: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Ziada (67)