عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«حَقُّ الْمُسْلِمِ عَلَى الْمُسْلِمِ سِتٌّ» قِيلَ: مَا هُنَّ يَا رَسُولَ اللهِ؟، قَالَ: «إِذَا لَقِيتَهُ فَسَلِّمْ عَلَيْهِ، وَإِذَا دَعَاكَ فَأَجِبْهُ، وَإِذَا اسْتَنْصَحَكَ فَانْصَحْ لَهُ، وَإِذَا عَطَسَ فَحَمِدَ اللهَ فَسَمِّتْهُ، وَإِذَا مَرِضَ فَعُدْهُ وَإِذَا مَاتَ فَاتَّبِعْهُ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2162]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Haki za muislamu juu ya muislamu mwenzake ni sita" Pakasemwa: Na ni zipi hizo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?, akasema: "Ukikutana naye msalimie, na akikuita muitikie, na akikutaka nasaha mnasihi, na akipiga chafya akamhimidi Mwenyezi Mungu basi muombee dua ya rehema, na akiugua mtembelee, na akifariki msindikize".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2162]
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa miongoni mwa haki za muislamu juu ya ndugu yake muislamu ni mambo sita: La kwanza: Amsalimie akikutana naye kwa kusema: Assalaam alaikum, naye atajibu salamu kwa kusema: Waalaikumussalaam. La pili: Kuitika wito wake atakapomuita kwa ajili ya sherehe ya harusi au nyingineyo. La tatu: Kumpa nasaha akizihitajia, na wala usimsifie bure, au kumfanyia udanganyifu. La nne: Akipiga chafya akasema: Alhamdulillaah, basi muombee dua kwa kusema: Yar-hamkallaah (Akuhurumie Mwenyezi Mungu), naye ajibu kwa kusema: Yah-diikumullaahu wayuslih baalakum (Akuongozeni Mwenyezi Mungu na kutengenezeeni hali zenu). La tano: Akamuone na amtembelee atakapougua. La sita: Amswalie atakapofariki, na alisindikize jeneza lake mpaka azikwe.