عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«انْظُرُوا إِلَى مَنْ أَسْفَلَ مِنْكُمْ، وَلَا تَنْظُرُوا إِلَى مَنْ هُوَ فَوْقَكُمْ، فَهُوَ أَجْدَرُ أَلَّا تَزْدَرُوا نِعْمَةَ اللهِ عَلَيْكُمْ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 2963]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema: Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Mtazameni aliyeko chini yenu, na wala msimtazame aliyeko juu yenu, kwa kufanya hilo, hilo litakufanyeni msidharau neema za Allah mlizonazo".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 2963]
Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemuamrisha muislamu kumtazama katika mambo ya dunia katika nafasi na mali na cheo na mengineyo yule ambaye ana hali ya chini zaidi, na asimtazame katika mambo ya dunia yake yule aliyeko juu yake na bora zaidi kuliko yeye, kwa kumtazama aliyeko chini ni bora na kunastahiki zaidi kumfanya asidharau na kuzidogesha neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yake.