عن النعمان بن بشير رضي الله عنه قال: سمعت النبي صلى الله عليه وسلم يقول: «إن الحلال بيِّن وإن الحرام بين، وبينهما أمور مُشْتَبِهَاتٌ لا يعلمهن كثير من الناس، فمن اتقى الشُّبُهات فقد اسْتَبْرَأ لدينه وعرضه، ومن وقع في الشبهات وقع في الحرام، كالراعي يرعى حول الحِمى يوشك أن يَرْتَع فيه، ألا وإن لكل مَلِك حِمى، ألا وإن حِمى الله محارمه، ألا وإن في الجسد مُضغة إذا صلحت صلح الجسد كله وإذا فسدت فسد الجسد كله ألا وهي القلب».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Nu'man bin Bashiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume rehema na Amani ziwe juu yake- Akisema: "Hakika halali iko wazi na hakika haramu iko wazi, na kati ya hayo kuna mambo yenye kutatiza hawayafahamu wengi katika watu, atakaye yaepuka mambo yenye kutatiza basi atakuwa ameitakasa dini yake na heshima yake, na atakayetumbukia katika mambo yenye kutatiza atakuwa katumbukia katika haramu, kama mchunga mifugo anayechunga kando kando ya mipaka anahofiwa (mifugo yake) kuingia humo, Tambueni kuwa kila mfalme ana mipaka, tambueni kuwa mipaka ya Mwenyezi Mungu ni yale aliyoyaharamisha, tambueni kuwa hakika katika kiwiwili kuna pande la nyama likitengemaa mwili mzima unatengamaa,na likiharibika unaharibika mwili mzima, Tambueni pande hilo ni moyo"
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Kanuni ya kiujumla nikuwa yote aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake yote kati ya hayo mawili yako wazi na yanaeleweka, ispokuwa kinachohofiwa kwa muislamu ni mambo yenye kutatiza, atakayeyaacha yale mambo yenye kutatiza kwake dini yake itakuwa imesalimika kwa kuwa mbali na kutumbukia katika haramu, na utakuwa umekamilika kwa hilo ulinzi wa heshima yake kutokana na maneno ya watu kwa yale wanayoweza kumdhalilisha kwayo kwasababu ya kuyafanya kwake haya yenye kutatiza. Na ambaye hatoyaepuka yenye kutatiza, basi atakuwa ameisogeza nafsi yake kutumbukia katika haramu, au watu kumsengenya na kuharibu heshima yake. Na amepiga Mtume rehema na Amani ziwe juu yake mfano kwa anayeyaendea yenye kutatiza kama anayechunga ngamia wake au mbuzi wake karibu na ardhi ambayo mwenye nayo ameiwekea mipaka, inahofiwa mifugo ya huyu bwana kulisha katika mipaka hii kwasababu ya ukaribu wake na mipaka hiyo, na hivyo hivyo mwenye kufanya yenye utata ndani yake, basi na yeye anaikaribia haramu ya wazi, anahofiwa kutumbukia ndani yake. Na akaashiria Mtume rehema na Amani ziwe juu yake kuwa matendo ya wazi ni dalili ya matendo ya ndani katika kutengemaa au kuharibika, akabainisha kuwa kiwiliwili ndani yake kuna pande la nyama (Nalo ni moyo) mwili unatengemaa kwa kutengemaa kwake na unaharibika kwa kuharibika kwake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kuhimizwa juu ya kufanya mambo ya halali na kuiepuka haramu na mambo yenye kutatiza.
  2. Mambo yenye kutatiza yana hukumu yake maalumu ambayo kuna dalili ya kisheria ambayo inawezekana baadhi ya watu wakayafikia hata kama yatafichikana kwa watu wengi.
  3. Ambaye hatoepuka utata katika chumo lake na maisha yake na miamala yake mingine atakuwa ameiingiza nafsi yake katika kusemwa vibaya.
  4. Kutanabahishwa juu ya kuupa heshima moyo na kuhimizwa juu ya kuurekebisha, kwani moyo ndio kiongozi wa mwili kwa kutengemaa kwake mwili unatengemaa, na kwa kuharibika kwakwe mwili unaharibika.
  5. Kugawanywa mambo kulingana na uhalali na uharamu katika migawanyiko mitatu: Halali ya wazi na Haramu ya wazi na yenye kutatiza.
  6. Kuhifadhi juu ya mambo ya dini na kulinda heshima.
  7. Kuziba njia zinazopelekea katika haramu, na ushahidi juu ya hilo ni mwingi.
  8. Kupigwa mifano ya maana ya kisheria na ya kielimu.