عن عمر بن الخطاب رضي الله عنه قال: إنه سمع نبي الله صلى الله عليه وسلم يقول:
«لَو أَنَّكُمْ تَتَوَكَّلُونَ عَلَى اللهِ حَقَّ تَوَكُّلِهِ، لَرَزَقَكُمْ كَمَا يَرْزُقُ الطَّيْرَ، تَغْدُو خِمَاصًا وَتَرُوحُ بِطَانًا».
[صحيح] - [رواه الترمذي وابن ماجه وأحمد] - [مسند أحمد: 205]
المزيــد ...
imepokewa Kutoka kwa Omari bin Khattwab -Radhi za Allah ziwe juu yake-: Hakika yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Lau kama nyinyi mngelimtegemea Mwenyezi Mungu ukweli wa kumtegemea, basi angekuruzukuni kama anavyomruzuku ndege, anatoka asubuhi akiwa na njaa anarudi mchana akiwa kashiba".
[Sahihi] - - [مسند أحمد - 205]
Anatuhimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuleta manufaa na kuzuia madhara katika mambo ya Dunia na Akhera, kwani hakuna yeyote mwenye kutoa wala kunyima wala kudhuru wala kunufaisha isipokuwa Yeye Aliyetakasika na Kutukuka, Na tufanye sababu zinazoleta manufaa na kuzuia madhara, pamoja na kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa dhati, wakati wowote tutakapofanya hivyo, Mwenyezi Mungu ataturuzuku kama anavyowaruzuku ndege wanaotoka asubuhi wakiwa na njaa, kisha wanarudi jioni matumbo yakiwa yamejaa, na kitendo hiki kwa ndege ni aina ya kufanya sababu za kutafuta riziki, bila kubweteka wala uvivu.