+ -

عَن ابنِ عباسٍ رضي الله عنهما أنَّ رسولَ اللهِ صلي الله عليه وسلم قال:
«لَو يُعطَى النّاسُ بدَعواهُم لادَّعَى رِجالٌ أموالَ قَومٍ ودِماءَهُم، ولَكِنَّ البَيِّنَةَ على المُدَّعِى، واليَمينَ على مَن أنكَرَ».

[صحيح] - [رواه البيهقي] - [السنن الكبرى للبيهقي: 21243]
المزيــد ...

Na imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume wa Mweyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Laiti wangepewa watu yote wanayodai basi kuna watu wangedai mali za wenzao na damu zao, lakini ushahidi ni kwa mwenye kudai na kiapo ni kwa mwenye kukanusha".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Albayhaqy] - [السنن الكبرى للبيهقي - 21243]

Ufafanuzi

Amebainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa lau watu wangelipwa kwa msingi wa madai yao tu, bila ya ushahidi wala vielelezo, basi watu watadai mali na damu za watu wengine, lakini mwenye kudai lazima awasilishe alama na ushahidi wa kile anachodai, ikiwa hana ushahidi basi madai hayo yanawasilishwa kwa mshitakiwa, na akikanusha ni lazima aape na kuachiliwa.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية الصربية الرومانية Luqadda malgaashka Luqadda kinaadiga الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Amesema bin Daqiq Al-Idd: Na hadithi hii ni msingi katika misingi ya utoaji wa hukumu, na ni marejeo makubwa wakati wa mzozo na ugomvi.
  2. Sheria imekuja kulinda mali za watu na damu zao zisichezewe.
  3. Hakimu asikuhumu kwa elimu yake bali arudi katika ushahidi.
  4. Yeyote atakayedai madai ambayo hayana uthibitisho yatakataliwa, iwe yanahusu haki na miamala au masuala ya imani na sayansi.