عن عائشة رضي الله عنها مرفوعاً: «لا تسبوا الأموات؛ فإنهم قد أفضوا إلى ما قدموا».
[صحيح] - [رواه البخاري]
المزيــد ...
Kutoka kwa Aisha Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, Hadithi Marfu'u: "Msiwatukane wafu: kwani wao tayari wameyaendea yale waliyoyatanguliza".
Sahihi - Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Hadithi hii ni dalili juu ya uharamu wa kuwatukana wafu na kujiingiza katika heshima zao, Nakuwa haya ni katika tabia mbaya, na hekima ya kukatazwa kwake imekuja katika kauli yake iliyobakia katika hadithi: "Kwani wao tayari wameyaendea yale waliyoyatanguliza" Yaani wameyafikia yale waliyoyatanguliza katika matendo yao mema au maovu, na matusi haya hayawafikii bali yanawaudhi waliohai.