Orodha ya Hadithi

Mwenye kuhiji na akawa hakusema maneno machafu wala kutenda matendo machafu, anarudi kama alivyo zaliwa na mama yake (akiwa hana dhambi).
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Utakaposema kumwambia mwenzio: Nyamaza siku ya ijumaa na Imamu ana khutubu, utakuwa umefanya mchezo.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Mambo ya kimaumbile ni matano: Kutairiwa, na kuondoa nywele za sehemu ya siri, na kupunguza masharubu, na kupunguza kucha, na kukwapua nywele za kwapani.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Ewe Mola wangu usilifanye kaburi langu kuwa ni sanamu lenye kuabudiwa, zimekuwa kali hasira za Mwenyezi Mungu juu ya watu walioyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa Misikiti.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Swala nzito juu ya wanafiki: ni swala ya ishaa na swala ya Alfajiri, na lau wangejua yaliyomo ndani ya swala hizo, basi wangeziendea hata kwa kutambaa, na nilitamani niamrishe swala ikimiwe, kisha nimuamrishe mtu awaswalishe watu, kisha niondoke wakiwa pamoja nami wanaume wakiwa na vijinga vya moto twende kwa watu ambao hawahudhurii swala nikazichome nyumba zao kwa moto.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Haikubali Mwenyezi Mungu swala ya mmoja wenu atakapotengukwa udhu mpaka atawadhe.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Swala tano, na Ijumaa mpaka Ijumaa, na ramadhani mpaka ramadhani vinafuta madhambi yaliyo kati yake, yatakapoepukwa madhambi makubwa.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakaye simama usiku wenye cheo (Lailatul Qadri) kwa imani na kwa kutaraji malipo, atasamehewa yaliyotangulia katika madhambi yake.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Msiwatukane wafu: kwani wao tayari wameyaendea yale waliyoyatanguliza
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakaye swali swala ya Al-fajiri atakuwa katika mkataba wa Mwenyezi Mungu hivyo asikutafuteni Mwenyezi Mungu katika mkataba wake kwa chochote
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Anasema: kila mwisho wa swala anapotoa salamu: "Laa ilaaha illa llaahu wahdahu Laa shariika lahu, Lahul Mulku walahul Hamdu wahuwa a'laa kulli shai in qadiir, Laa haulaa walaa quwwata illaa billaah, walaa na'budu illaa iyyaahu, Lahun ni'matu walahul Fadhlu, walahuth thanaaul hasan, Laa ilaaha Illa llaahu Mukhliswiina lahud diina walau karihal kaafiruun" Yaani: Hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika, Ufalme ni wake na sifa njema ni zake, naye juu ya kila kitu ni muweza, Hakuna ujanja wala nguvu ila kwa Mwenyezi Mungu, Hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu, Na hakuna tunayemuabudu ila yeye, ana neema na ana fadhila, na ana sifa njema, Hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu tunamtakasia dini hata kama makafiri watachukia.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakuna siku ambazo matendo mema yanapendeka zaidi ndani yake kwa Mwenyezi Mungu kama masiku haya.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayeacha swala ya Laasiri itakuwa imeporomoka amali yake.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu, yatatoka madhambi yake mwilini mwake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Jisafisheni vizuri kutokana na mkojo; kwani adhabu nyingi za kaburini zinatokana na hilo.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Msiswali makaburini, wala msiyakalie makaburi.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hao ni watu ambao anapokufa kwao mja mwema, au mtu mwema, wanajenga juu ya kaburi lake msikiti, na wanachora hapo mapicha, hao ni viumbe waovu mbele ya Mwenyezi Mungu.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nimeamrishwa nisujudu kwa viungo saba, kwa paji la uso, na akaashiria kwa mkono wake katika pua yake, na mikono miwili na magoti mawili, na ncha za miguu miwili, na wala tusizikunje nguo na nywele
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Yakuwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- Alikuwa akisema kati ya sijida mbili: Allaahumma ghfirlii, warhamnii, wa aafinii, wahdinii. warzuqnii (Ewe Mola wangu nisamehe, na unirehemu, na unipe afya, na uniongoze, na uniruzuku)
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehma na Amani ziwe juu yake- anapomaliza swala yake anataka msamaha mara tatu, na anasema: Allaahumma antas salaam, waminkas salaam, Tabaarakta yaa dhal-jalaali wal-ikraam (Ewe Mwenyezi Mungu hakika wewe ni Amani, na Amani hutoka kwako, umetakasika Ewe mwenye Utukufu na ukarimu).
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Swali ukiwa umekaa, ikiwa hutoweza basi ukiwa umekaa, ikiwa hutoweza basi ukiwa umelalia ubavu.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Alimuijia Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake mtu kipofu, Akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika sina muongozaji wa kuniongoza njia kuja msikitini, akamuomba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake amruhusu aswalie nyumbani kwake, akamruhusu, alipogeuka kuondoka akamuita, kisha akasema: Je unasikia wito wa swala? Akasema: Ndiyo, akasema: basi itikia wito wa sala.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakapokuja mmoja wenu katika swala na imamu akawa yuko katika hali fulani, basi na afanye kama anavyofanya
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayemuua aliyechukua ahadi ya kulindwa, hatonusa harufu ya pepo, na hakika hurufu yake hupatikana kuanzia mwendo wa miaka arobaini.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Umejengwa uislamu kwa mambo matano
عربي Lugha ya kiingereza Kiispania
Kutosheka na mambo ya wajibu.
عربي Lugha ya kiingereza Kiispania
Twahara (usafi) ni sehemu ya imani
عربي Lugha ya kiingereza Kiispania
Ibada ya Umra ndani ya ramadhani inalingana na Hija -au Hija pamoja nami.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Alikuwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akikaa itikafu katika kila ramadhani siku kumi, ulipofikia mwaka aliofishwa ndani yake alikaa itikafu siku ishirini
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Kwenu nyinyi jihadi bora: ni hija njema
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Yakwamba mwanamke mmoja alipatikana katika baadhi ya vita vya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akiwa kauwawa
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayepigana ili liwe neno la Mwenyezi Mungu ndio la juu basi huyo yuko katika njia ya Mwenyezi Mungu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Mtakapomsikia muadhini basi semeni mfano wa jinsi anavyosema
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nilikuwa pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika safari, nikanyoosha mikono ili nimvue viatu vyake (khufu), akasema; ziache; kwani hakika mimi nimezivaa zikiwa safi, akafuta juu yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Yakwamba Fatuma bint Abii Hubaishi: Alimuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Akasema: Hakika mimi napata hedhi na wala sitwahariki, je niache swala? Akasema: Hapana usiache sala, Hakika huo niupasukaji wa mshipa, lakini acha swala kiasi cha siku ambazo ulikuwa ukiingia katika hedhi, kisha oga na uswali
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nyoosheni safu zenu, kwani hakika kunyoosha safu ni katika ukamilifu wa swala
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakapotawadha mmoja wenu basi na aweke puani mwake maji, kisha apenge, na atakayestanji kwa mawe basi ayafanye kuwa witiri, na atakapoamka mmoja wenu toka usingizini mwake basi na aoshe mikono yake kabla hajaiingiza katika chombo mara tatu, kwani hakika mmoja wenu hajui ni wapi ulilala mkono wake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nilisali pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- rakaa mbili kabla ya adhuhuri, na rakaa mbili baada yake, na rakaa mbili baada ya Ijumaa, na rakaa mbili baada ya magharibi, na rakaa mbili baada ya ishaa
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapoamka asubuhi anasukutua kinywa chake kwa mswaki
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Paliletwa mashtaka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuhusu mtu anayepata wasiwasi kuwa anapata kitu ndani ya swala (katika vitenguzi vya udhu), Akasema: asiondoke mpaka asikie sauti, au apate harufu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Itakaposimamishwa swala na kikatengwa chakula cha usiku basi anzeni na chakula cha usiku
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nilikuwa pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akaenda haja ndogo, akatawadha, na akafuta juu ya khufu zake (viatu vya ngozi mfano wa soksi).
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Mtakapokwenda haja kubwa, msielekee kibla kwa haja kubwa wala ndogo, na wala msikipe kibla mgongo, lakini elekeeni mashariki au magharibi.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Asishike mmoja wenu utupu wake kwa mkono wake wa kulia akiwa anakidhi haja ndogo, na asijifute haja ndogo au kubwa kwa mkono wake wa kulia na asipumulie ndani ya chombo anachonywea.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Amekataza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuswali baada ya swala ya sub-hi mpaka lichomoze jua, na baada ya laasiri mpaka lizame
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hivi haogopi mmoja wenu anayenyanyua kichwa chake kabla ya imamu Mwenyezi Mungu kukigeuza kichwa chake kuwa kichwa cha punda, au aifanye sura yake kuwa sura ya punda?
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Alikuwa akinyanyua mikono yake usawa wa mabega yake anapofungua swala, na anapotoa takbira ya kurukuu, na anaponyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu anainyanyua pia
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Alinifundisha mimi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- tashahudi (tahiyatu), mkono wangu ukiwa katikati ya mikono yake kama anavyonifundisha sura katika Qur'ani
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akiomba: Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na adhabu za kaburi, na adhabu ya moto, na mitihani ya uhai na kifo, na fitina za masihi dajali.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nimuweka fidia baba yangu na mama yangu, Hebu nieleze kunyamaza kwako kati ya takbira na kisomo: Ni nini unasema: Akasema: Ninasema: Allaahumma baaid bainiy -Ewe Mwenyezi Mungu weka mbali baina yangu- wa baina khatwaayaaya -na baina ya makosa yangu- kamaa baa a'tta bainal mashriqi wal maghribi -kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi. Allaahumma naqqiniy- Ewe Mwenyezi Mungu nitakase mimi- min khatwaayaaya -kutokana na makosa yangu- kamaa yunaqqaath-thaubul abyadhwa -kama inavyotakaswa nguo nyeupe- minad danasi -kutokana na uchafu. Allaahumma ghsilniy -Ewe Mwenyezi Mungu nioshe mimi- min khatwaayaaya -kutokana na makosa yangu- bil maai wath thalji wal baradi -kwa maji na barafu na baridi.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Linganeni sawa katika sijida, na asikunjue mmoja wenu mikono yake kama anavyokunjua mbwa
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nilimuuliza Anas bin Malik: alikuwa Nabii Rehema na amani za Allah ziwe juu yake- akiswali na viatu vyake? akasema: ndio
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakapokunywa mbwa katika chombo cha mmoja wenu basi akioshe mara saba
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na mashetani wa kiume na mashetani wa kike.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayemuomba Mwenyezi Mungu shahada (yaani kufa shahidi) kwa ukweli, basi atamfikisha daraja ya mashahidi hata kama atafia juu ya godoro lake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Waliamrishwa watu kuwe kuagana kwao kwa mwisho ni katika nyumba (Alka'ba), isipokuwa likaondoshwa hilo kwa mwanamke mwenye hedhi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Kiliwekwa kwaajili ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- chombo cha kuogea janaba, akamimina kwa mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto mara mbili -au tatu- kisha akaosha tupu yake, kisha akapiga ardhi kwa mkono wake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapooga janaba, anaosha mikono yake kisha anatawadha udhu wake wa swala kisha anaoga
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Msilifanye kaburi langu kuwa sikukuu, wala nyumba zenu kuwa makaburi, na nitakieni rehma, kwani dua zenu hunifikia popote mlipo
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nilikuwa ni mtu mwenye madhii mengi, nikaona haya kumuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwasababu ya nafasi ya binti yake kwangu, nikamtuma Mikidadi bin Aswadi akamuuliza, akasema: Ataosha tupu yake, na atatawadha
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Mtakapo vaa, na mtakapo tawadha, basi anzeni na kuliani kwenu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nilimuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ni amali ipi inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu? Akasema: Ni (kuiswali) swala kwa wakati wake. Nikasema: kisha nini? Akasema: Ni kuwatendea wema wazazi wawili
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakuna siku ambayo wanaamka ndani yake waja isipokuwa kuna Malaika wawili wanateremka,anasema mmoja wao: Ewe Mwenyezi Mungu mpe mtoaji badala,na anasema mwingine:Ewe Mwenyezi Mungu mpe mzuiaji hasara
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakaye muandaa mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu basi na yeye atakuwa kapigana, na atakayemsimamia mpiganaji katika familia yake basi na yeye atakuwa kapigana
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nilimshuhudia Amru bin Abii Hasan alimuuliza Abdullah bin Zaidi kuhusu udhu wa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akaagiza bakuli la maji, akatawadha kwaajili yao udhu wa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hivi hukujua kuwa uislamu hufuta madhambi yaliyokuwa kabla yake, na kuwa kuhama kunafuta madhambi yaliyokuwa kabla yake, nakuwa Hija inafuta madhambi yaliyokuwa kabla yake?
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nilimjia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- naye akiwa anapiga mswaki kwa mswaki wa mti mbichi, Akasema: na ncha ya mswaki ikiwa katika ulimi wake, naye akisema: AAGH, AAGH (sauti ya kujigogoa), na mswaki ukiwa mdomoni mwake, kana kwamba anajigogoa
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika inakutosheleza kusema kwa mikono yako hivi: kisha akapiga kwa mikono yake miwili chini ya ardhi mpigo mmoja, kisha akapaka mkono wa kulia kwa kutumia mkono wa wa kushoto, na akapaka juu ya viganja vyake na uso wake.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Na hakuna Nabii aliyetumwa na Mwenyezi Mungu katika umma wowote kabla yangu, isipokuwa anakuwa katika umma wake na watu wake wapendwa na watu wanaoyachukua mafundisho yake na wanafuata amri yake, kisha wanakuja kutofautiana baada yao watu wanaowafuata, wanazungumza yale wasiyoyafanya, na wanafanya ambayo hawakuamrishwa
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Yakwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na mguu wake ukiwa tayari umeuweka kwenye kipandwa (yaani yuko tayari kwa safari): Ni jihadi ipi bora? Akasema: ni neno la haki kwa kiongozi muovu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nilimpa utiifu Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- juu ya kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kumnasihi kila muislamu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Ewe Mu'adhi, Wallahi hakika mimi ninakupenda, kisha ninakuusia ewe Mu'adhi, hakikisha usiache mwisho wa kila swala kusema: Allaahumma ainniy alaa dhikirika -Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie mimi niweze kukutaja wewe, Washukurika- na kukushukuru, Wahusni ibaadatika -Na kuzifanya vizuri ibada zako.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Adhabu kali ya moto itazipata nyayo za miguu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Alichelewesha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- swala ya ishaa, akatoka Omar, akasema: Swala Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wamelala wanawake na watoto, akatoka na kichwa chake kikitona maji akisema: Lau kama nisingehofia kuwapa tabu umma wangu basi ningewaamrisha swala hii waiswali wakati huu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Amesema Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka-: Kila amali ya mwanadamu hiyo ni ya kwake isipokuwa swaumu, bila shaka hiyo ni yangu na mimi ndiye ninayeilipa.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Simama na uswali witiri ewe Aisha
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Allaahumma inni Audhubiridhwaaka min sakhatwika, -Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwa radhi zako kutokana na hasira zako, wabimuaafaatika min uquubatika,- Na kwa msamaha wako kutokana na adhabu zako-, Wa a'udhubika minka, -na ninajilinda kwako kwa ulinzi utokao kwako-, Laa uhswith thanaa 'alaika, -Siwezi kuzidhibiti shukurani zote juu yako, Anta kamaa athnaita a'laa nafsika, -Wewe kama ulivyojisifia nafsi yako
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Aliulizwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: Ni swala ipi bora? Akasema: Ni kurefusha kisimamo
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Ni kwa jambo lipi alikuwa akianza nalo Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Anapoingia nyumbani kwake? Akasema: kwa mswaki
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Huyo mtu kamkojolea shetani masikioni mwake, au alisema: sikioni kwake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Mambo kumi ni katika maumbile: Kupunguza masharubu, na kuziachia ndevu,na kupiga mswaki, na kupandisha maji puani, na kupunguza kucha, na kuosha fundo za vidole, na kunyofoa nywele za makwapani, na kunyoa nywele za sehemu za siri, na kustanji kwa maji.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Anafunga shetani juu ya kisogo cha kichwa cha mmoja wenu, pindi anapolala, mafundo matatu, anapiga katika kila fundo: Unatakiwa kulala usiku mrefu basi lala
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Shikamana na kukithirisha kusujudu; kwani wewe hutosujudu kwaajili ya Mwenyezi Mungu sijida moja isipokuwa atakunyanyua Mwenyezi Mungu kwa hiyo sijida daraja moja, na anakufutia kwa hiyo dhambi moja
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akifanya juhudi katika ramadhani kwa namna ambayo hajitahidi katika nyakati zingine nje ya ramadhani, na katika kumi la mwisho pia alikuwa na juhudi ambazo hakuwa anajitahidi hivyo nje ya ramadhani
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Tulikuwa tukimuandalia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- mswaki wake na (maji yake kwaajili ya) twahara, basi Mwenyezi Mungu anamuamsha kwa muda anaotaka aamke nyakati za usiku, anapiga mswaki, na anatawadha na anaswali
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Haijawahi kupata vumbi miguu ya mja yeyote katika njia ya Mwenyezi Mungu, halafu ikaguswa na moto
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Anachokipata aliyekufa shahidi katika maumivu ya kifo, ni kama maumivu anayoyapata mmoja wenu kutokana na kung'atwa na mdudu chungu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayeswali (katika nyakati mbili) za baridi ataingia peponi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hivi unaonaje ikiwa nitauwawa katika njia ya Mwenyezi Mungu, je yatafutwa makosa yangu?
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa