+ -

عَنْ أَنَسٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ:
كَانَتْ عَامَّةُ وَصِيَّةِ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حِينَ حَضَرَهُ الْمَوْتُ: «الصَّلَاةَ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ، الصَّلَاةَ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ»، حَتَّى جَعَلَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُغَرْغِرُ بِهَا صَدْرُهُ، وَمَا يَكَادُ يُفِيضُ بِهَا لِسَانُهُ.

[صحيح] - [رواه النسائي في السنن الكبرى وابن ماجه] - [مسند أحمد: 12169]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Anas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake amesema:
Ulikuwa usia mkubwa wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipofikwa na mauti: "(Shikamaneni na) Swala nyinyi na waliomilikiwa na mikono yenu ya kuume, (Shikamaneni na) Swala nyinyi na waliomilikiwa na mikono yenu ya kuume", mpaka akaanza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kushikwa na kwikwi kifuani kwake kwa maneno hayo kwa sababu ya kifo, na maneno hayo yalikaribia kujaa ulimi wake.

[Sahihi] - - [مسند أحمد - 12169]

Ufafanuzi

Ulikuwa usia mwingi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Umma wake naye akiwa katika ulevi wa kifo: Shikamaneni na swala na mdumu nayo na wala msighafilike nayo, na vile vile timizeni haki za wale wanaomilikiwa na mikono yenu ya kuume miongoni mwa watumwa na wajakazi na wamilikini kwa wema, akaendelea kuukariri, mpaka ukaanza kumkwama katika koo lake, na ulimi wake ukashindwa kuutamka kwa ufasaha.

Tafsiri: Lugha ya Kiindonesia Kisin-hala Kivetenamu Kihausa Thai Kiassam الأمهرية الهولندية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Ukubwa wa jambo la swala na haki ya mamluki; kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliusia mambo hayo mawili katika mwisho wa yale aliyousia.
  2. Swala ni katika haki kubwa za Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na kutimiza haki za viumbe na hasa hasa madhaifu, nao ni wale waliochini ya mkono wa mtu wasiokuwa kizazi chake nalo ni katika haki kubwa za viumbe.