عن بريدة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
«إِنَّ الْعَهْدَ الَّذِي بَيْنَنَا وَبَيْنَهُمُ الصَّلَاةُ، فَمَنْ تَرَكَهَا فَقَدْ كَفَرَ».

[صحيح] - [رواه الترمذي والنسائي وابن ماجه وأحمد] - [سنن النسائي: 463]
المزيــد ...

Kutoka kwa Buraida -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Hakika ahadi iliyopo kati yetu na wasiokuwa waislamu ni sala, na atakayeiacha sala basi huyo ni kafiri".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na Ahmad] - [Sunanu Al Nasaai - 463]

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa ahadi na mkataba kati ya waislamu na wasiokuwa wao katika makafiri na wanafiki ni swala, atakayeiacha atakuwa amekufuru.

Katika Faida za Hadithi

  1. Ukubwa wa jambo la swala, nakuwa ndio kitenganishi kati ya waumini na makafiri.
  2. Kudhihiri hukumu za Uislamu kwa muonekano wa hali ya mtu pasina ndani ya moyo wake.
Kuonyesha Tarjama
Lugha: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Ziada (57)