عن ابن عباس رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : "من اقتَبَس شُعْبَة من النُّجوم؛ فقد اقتَبَسَ شُعْبة من السِّحْر، زاد ما زاد".
[صحيح] - [رواه أبو داود وابن ماجه وأحمد]
المزيــد ...

Kutoka kwa Ibn Abbasi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu- Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Atakayejifunza sehemu katika elimu ya nyota; basi atakuwa kajifunza sehemu katika uchawi, amezidisha anavyozidisha". Yaani: kila anavyozidi kujifunza ndivyo anavyozidisha uchawi.
Sahihi - Imepokelewa na Ibnu Maajah

Ufafanuzi

Na kwakuwa ilivyo, ghaibu ni katika mambo ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu- ameyabakisha kwake- Amebatilisha Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- kila jaribio la kutaka kubaini na kuchungulia katika siri zake, na miongoni mwa hayo ni elimu ya nyota- Ambayo ni kutoa ushahidi kupitia hali ya anga juu ya matukio ya ardhini, amebainisha Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa kujifunza hili ni aina ya uchawi, nakuwa kila anavyozidisha mtu jambo basi anakuwa kazidisha uchawi.

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kichina Kifursi Kihindi Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto
Kuonyesha Tarjama

من فوائد الحديث

  1. Uharamu wa elimu ya nyota ambayo ni kutoa taarifa ya matukio yajayo kwa kutegemea hali za nyota; kwasababu hilo ni katika kudai kujua elimu ya ghaibu.
  2. Nikuwa elimu ya nyota ni katika aina za uchawi unaopingana na tauhidi.
  3. Nikuwa yeye kila anavyozidi kujifunza elimu ya nyota ndivyo anavyozidi kujifunza uchawi.
  4. Nikuwa uchawi unagawanyika.