عن بعض أزواج النبي صلى الله عليه وسلم عن النبي صلى الله عليه وسلم قال:
«مَنْ أَتَى عَرَّافًا فَسَأَلَهُ عَنْ شَيْءٍ لَمْ تُقْبَلْ لَهُ صَلَاةٌ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2230]
المزيــد ...
Kutoka kwa baadhi ya wake za Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- amesema:
"Atakayemuendea mpiga ramli akamuuliza kuhusu lolote hazitokubaliwa sala zake siku arobaini".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2230]
Anatahadharisha Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- kuwaendea wapiga ramli na hili ni jina la kiujumla la kuhani na mtabiri wa nyota na mpiga ramli na mfano wao, katika wale wanaotumia ishara za vitanguliza ili kudai kujua elimu ya ghaibu, nakuwa kumuuliza pekee mambo ya ghaibu Mwenyezi Mungu atamnyima thawabu za swala yake siku arobaini; na hiyo ni adhabu kwake kwa kosa hili na dhambi kubwa.