عن أبي عبد الله جابر بن عبد الله الأنصاري رضي الله عنهما أن رجلاً سأل رسول الله صلى الله عليه وسلم فقال: أرأيت إذا صليت المكتوبات، وصمت رمضان، وأحللت الحلال، وحرمت الحرام، ولم أزد على ذلك شيئاً، أأدخل الجنة؟ قال: «نعم».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Abdillahi Jabiri bin Abdillahi Al Answari Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, yakwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akasema: Unaonaje kama nitaswali swala za faradhi, na nikafunga ramadhani, na nikahalalisha halali na nikaharamisha haramu, na nikawa sikuzidisha zaidi ya hapo chochote, Je, naweza kuingia peponi? Akasema: "Ndiyo".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim
Amepokea Abuu Abdillahi Jabiri bin Abdillahi Al Answari Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, yakwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Akasema: Unaonaje: Yaani: Nieleze ikiwa nitaswali swala za faradhi, yaani swala tano za lazima, na nikawa sikuzidisha juu yake swala za sunna, na nikafunga ramadhani pekee bila kuongeza funga za sunna, na nikahalalisha halali, yaani nikafanya yale ya halali pamoja na kuharamisha haramu, yaani nikajiepusha na nikajiweka mbali nikiamini uharamu wake, nikatosheka na halali pekee, na nikawa sikuzidisha zaidi ya hapo chochote, Je, hilo linaweza kutosha kuingia peponi? Akajibu Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- (Ndiyo), kwasababu maana ya uchamungu ni kufanya maamrisho na kuacha makatazo, na mtu wa namna hii ndiye anayejulikana katika maandiko kuwa ni (Muqtaswid) aliyetosheka, naye ni yule asiyezidisha katika yale aliyomuwajibishia Mwenyezi Mungu juu yake, na haachi zaidi ya yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu juu yake.