عن أبي مالك الحارث بن الأشعري رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «الطهور شطر الإيمان، والحمد لله تملأ الميزان، وسبحان الله والحمد لله تملآن -أو تملأ- ما بين السماء والأرض، والصلاة نور، والصدقة برهان، والصبر ضياء، والقرآن حجة لك أو عليك، كل الناس يغدو: فبائعٌ نفسَه فمُعتِقُها أو مُوبِقها».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abii Maaliki Harithi bin Ash'ariy Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Twahara (usafi) ni sehemu ya imani, na (neno) Al hamdulillaah (kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu) hujaza mizani, na Sub-haanallaah na Al hamdulillaah vinajaza -au hujaza- yaliyo baina ya mbingu na ardhi, na swala ni nuru, na sadaka ni hoja, na subira ni mwangaza, na Qur'ani ni hoja ya kukutetea au kukukandamiza, watu wote hutoka asubuhi: kuna mwenye kuiuza nafsi yake akaiacha huru au akaiangamiza".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake kuwa usafi ni sehemu ya imani, na makusudio ya usafi ni kujisafisha, na twahur (usafi) ni maji yanayotumika kujisafishia, lakini makusudio yake ni kitendo cha kujisafisha, na inakusudiwa usafi wa nje na usafi wa ndani: kuvisafisha viungo kwa kuepuka najisi na kuondoa hadathi (uchafu usiyoonekana kama janaba), Na kuusafisha moyo kutokana na ushirikina na maradhi ya moyo (kama unafiki), Na maana ya sehemu ya imani: Yaani: ni nusu ya swala, kwasababu swala haikubaliki bila twahara, na akaeleza kuwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kunajaza mizani, Al hamdulillaahi ni kumsifia Mola Aliyetakasika na kutukuka kwa sifa za ukamilifu wake na sifa za utukufu wake pamoja na kumpenda na kumtukuza, hii hujaza mizani ambayo hupimia matendo, Na sub-haanallaah (Ametakasika Mwenyezi Mungu) ni kumtakasa Mwenyezi Mungu na yale yote yasiyofaa kwake miongoni mwa aibu na kufanana na viumbe, na maneno; Sub-haanallaah na Al hamdulillaah yanajaza au hujaza, yaani hapa hii ni shaka ya mpokezi, je Mtume alisema yanajaza au hujaza?!, baina ya mbingu na ardhi ni mwendo wa miaka mia tano ni neno moja au yote mawili yanajaza nafasi hiyo; kwasababu fadhila za Mwenyezi Mungu haziwekewi kikomo, Na swala ni nuru; ni nuru duniani na ni nuru ya mja siku ya kiyama, Na sadaka ni hoja, yaani ni hoja ya wazi juu ya ukweli wa imani ya mtoaji wake; kwasababu nafsi zimeumbwa kupenda mali, kitendo cha mtu kutoa mali hiyo kwa roho safi, hakuna shaka kuwa hii ni alama ya wazi na ni hoja ya wazi juu ya ukweli wa imani yake, na subira ni mwangaza kwa aina zake tatu: Subira katika kumtii Mwenyezi Mungu, na kusubiri katika maasi, na kusubiri juu ya makadirio ya Mwenyezi Mungu yenye kuumiza, basi hiyo ni mwangaza unao mwangazia njia mfanyaji wake. Na Qur'ani ni hoja ya kukutetea au kukukandamiza, Qur'ani ni maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyoteremshwa juu ya Nabii wake -Rehema na Amani ziwe juu yake- kupitia Jibrili, yaliyohifadhiwa katika kurasa, maneno ambayo atakayesimama kuyasoma ni kana kwamba anazungumza na Al Rahmaan (Mwingi wa Rehema), Hivyo haikwepeki ima yawe ni hoja kwako ya kukutetea, utakapoyaamini na kusadikisha yote yaliyomo, ukiyafanyia kazi maamrisho yake, na ukiyaepuka makatazo yake, kwa hili Qur'ani inakuwa ni mtetezi kwako siku ya kiyama, au ikukandamize, utakapoichukua na ukaihifadhi kisha ukalala, na ukalala pia usiswali, au ukafanya yanayokwenda kinyume na maamrisho yake na makatazo yake, basi hapo inakuwa ni hoja ya kukukandamiza juu yako. Watu wote hutoka asubuhi: Yaani: watu wote wakiamka hutawanyika katika ardhi kutafuta riziki, lakini baadhi ya watu kutoka kwao ni kwa ajili ya masilahi ya nafsi zao, na baadhi ya watu kutoka kwao ni kuziangamiza nafsi zao, na wote hao wanaziuza nafsi zao: Yaani matendo ndiyo yanayoziangamiza, Hivyo ima umuuzie Mwenyezi Mungu Mtukufu, uiokoe na moto wake, au umuuzie shetani kwa kufanya maasi na makosa na machafu uiangamizie motoni.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Kiispania Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kirashia Kibangali Kifursi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Kikurdi Kireno Kimalayo Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Pashto Kiassam Albanian
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Hii ni katika ukamilifu wa mazungumzo yake ziwe juu yake sala na salamu.
  2. Umuhimu wa kujisafisha nje na ndani.
  3. Ubora wa kumtaja Mwenyezi Mungu Mtakasifu na Mtukufu.
  4. Huruma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu pale alipoweka kutoka katika maneno mepesi malipo makubwa.
  5. Umuhimu wa kudumisha swala kwani hiyo ni nuru kwa mja duniani na siku ya kiyama.
  6. Sadaka ni alama ya imani ya kweli.
  7. Umuhimu wa kuifanyia kazi Qur'ani na kuiamini ili iwe ni hoja ya kukutetea na si ya kukukandamiza.
  8. Nikuwa uhuru wa kweli ni kusimama katika kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu, na si mtu ajiachie mwenyewe afanya kila anachokitaka.
  9. Nikuwa mwanadamu ni lazima afanye lolote ima la kheri au la shari.