عن المقدام بن معدِيْكَرِب قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: (ألا هل عسى رجلٌ يبلغه الحديث عني وهو متكئ على أريكته فيقول: بيننا وبينكم كتاب الله، فما وجدنا فيه حلالًا استحللناه، وما وجدنا فيه حرامًا حرمناه. وإن ما حرم رسول الله كما حرم الله).
[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي وابن ماجه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Mikidadi bin Ma'diyakrib amesema: Amesema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Alaah! Tambueni zimekaribia zama mtu yatamfikia mazungumzo toka kwangu naye akiwa kakaa kitandani kwake na aseme: baina yetu na nyinyi ni kitabu cha Mwenyezi Mungu, tutakachokipata kuwa ni cha halali basi tutakihalalisha, na tutakachokikuta ni cha haramu tutakiharamisha. Na hakika aliyoyaharamisha Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni sawa na aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu".
Sahihi - Imepokelewa na Ibnu Maajah

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- miongoni mwa makundi ya watu hawazitukuzi hadithi zake Rehema na amani ziwe juu yake, na miongoni mwao hawatumii sunna zake kama hoja na hawazijali, na mmoja kati yao ikimfikia hadithi miongoni mwa hadithi zake rehema na amani ziwe juu yake, naye akiwa ameegemea katika kitanda chake anakataa na anasema: baina yetu na nyinyi ni Qur'ani, tutakalo likuta ni halali tunalihalalisha, na tutakalo likuta ni haramu tunaliharamisha, naye haifanyii kazi na haamini kile alichofikishiwa katika hadithi na anafanya kwa madai yake Qur'ani kuwa ndiyo msingi wake, na lau kama angeifanyia kazi Qur'ani angeshikamana na sunna, kwa sababu Qur'ani imeamrisha kumtii Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake, na wale walionukuu sunna ndio walio nukuu Qur'ni, na ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kuwa alicho kiharamisha Mwenyezi Mungu na alichoharamisha Mtume wake ni sawa sawa, na kuharamisha kwa Mtume ni kuharamisha kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu yeye ni mfikishaji kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wala hatamki kwa matamanio ziwe juu yake Rehema na Amani.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Kiispania Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kirashia Kibangali Kifursi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Kikurdi Kireno Kimalayo Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Pashto Kiassam Albanian
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kuheshimu maneno ya Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake, na kuheshimu amri zake na makatazo yake.
  2. Nikuwa kufanya hivyo ni kuiheshimu Qur'ani Tukufu.
  3. Aliyoyaharamisha Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake hayo ni katika yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu.
  4. Kupingana na Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake ni sawa na kumpinga Mwenyezi Mungu -Mtukufu-.
  5. Nikuwa atakayepuuza mafundisho ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na akadai kutosheka na Qur'ani basi atakuwa kavipuuza vyote na atakuwa muongo katika madai ya kufuata Qur'ani.