Orodha ya Hadithi

Namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hatonisikia yeyote katika umma huu, Myahudi wala Mkristo, kisha akafa haliyakuwa hajayaamini yale niliyotumwa kwayo, ispokuwa atakuwa ni katika watu wa motoni.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Laana za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Mayahudi na Wakristo, waliyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa misikiti- Anatahadharisha waliyoyafanya- na lau isingekuwa kauli hiyo basi lingedhihirishwa kaburi lake, (Angezikwa nje) ispokuwa alihofia kufanywa kuwa msikiti.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Ewe Mola wangu usilifanye kaburi langu kuwa ni sanamu lenye kuabudiwa, zimekuwa kali hasira za Mwenyezi Mungu juu ya watu walioyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa Misikiti.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika ukubwa wa malipo huendana sawa pamoja na ukubwa wa matatizo, na hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anapowapenda watu huwapa mtihani; atakayeridhia atapata radhi, na atakayechukia atapata hasira (za Mwenyezi Mungu).
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Mimi nimejitosheleza na washirika juu ya kushirikishwa; atakayefanya jambo lolote akamshirikisha pamoja nami mwingine nitamuacha na shirki yake au (na mshirika wake).
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika mimi najiepusha kwa Mwenyezi Mungu kuwa kwangu kati yenu na rafiki wa ndani, kwani Mwenyezi Mungu amenifanya mimi kuwa kipenzi wa ndani kama alivyomfanya Ibrahim kuwa kipenzi wa ndani, na lau kama ningejifanyia kipenzi wa ndani katika umma wangu basi ningemfanya Abuubakari kuwa kipenzi wa ndani.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anapata wivu, na wivu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, ni kuyafanya mtu yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu kwake yeye.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Mwenye kumuapia asiyekuwa Allah atakuwa amekufuru au kamshirikisha Allah .
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Swala nzito juu ya wanafiki: ni swala ya ishaa na swala ya Alfajiri, na lau wangejua yaliyomo ndani ya swala hizo, basi wangeziendea hata kwa kutambaa, na nilitamani niamrishe swala ikimiwe, kisha nimuamrishe mtu awaswalishe watu, kisha niondoke wakiwa pamoja nami wanaume wakiwa na vijinga vya moto twende kwa watu ambao hawahudhurii swala nikazichome nyumba zao kwa moto.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika katika watu waovu ni wale kitakaowakuta kiyama wakiwa hai, na wale wanaoyafanya makaburi kuwa ni misikiti.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Ninaloliogopea zaidi kwenu nyinyi: ni shirki ndogo, akaulizwa kuhusu hilo, akasema: ni Riyaa (kujionyesha).
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Kwani hawaharamishi aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu nanyi mkayaharamisha? na wanahalalisha aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu nanyi mkayahalalisha? Nikasema: Ndivyo, Akasema: Basi huko ndiko kuwaabudu.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika wewe unawaendea watu wa kitabu, basi naliwe la mwanzo utakalowaita kwalo ni kushuhudia kuwa hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Yakwamba Mtume rehema na Amani zimfikie aliulizwa kuhusu Nushra (kutibu uchawi kwa uchawi)? Akasema: Hiyo ni katika kazi za shetani.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
"Msichupe mipaka katika kunisifu kama walivyochupa mipaka manaswara kwa mwana wa Mariam, bila shaka hakika mimi ni mja wake, basi semeni; mja wa Mwenyezi Mungu na mjumbe wake"
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Ni nani atakayefurahika zaidi kwa utetezi wako? Akasema: Atakayesema Laa ilaaha illa llaahu (Hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu) kwa nia safi toka moyoni mwake.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Itakayemrudisha imani ya mkosi wa ndege akaacha shida yake basi atakuwa amefanya shirki, wakasema: Ni ipi kafara ya hilo? Akasema: ni useme: Ewe Mwenyezi Mungu hakuna kheri ila kheri yako, na hakuna ndege ispokuwa ndege wako, na hakuna Mola zaidi yako.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakaye shuhudia kuwa hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika nakuwa Muhammadi ni mjumbe wake na ni mja wake, nakuwa Issa ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na neno lake alilolipeleka kwa Mariam na ni roho toka kwake, na pepo ni kweli na moto ni kweli, Atamuingiza Mwenyezi Mungu peponi kulingana na yale aliyokuwa nayo katika matendo.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayekutana na Mwenyezi Mungu hali yakuwa hamshirikishi na chochote ataingia peponi, na atakaye kutananaye hali yakuwa anamshirikisha na chochote ataingia motoni.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayekufa naye akiomba kinyume na Mwenyezi Mungu mshirika, ataingia motoni
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Wameangamia wenye kujilazimisha -Alilisema hilo mara tatu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:- "Na wakasema msiwaache waungu wenu, wala msimuache Wadda, wala Suwa'u wala Yaghuth na Yauq na Nasr" Amesema Ibn Abbas Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Haya ni majina ya watu wema katika watu wa Nuhu.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayempa muda mwenye hali ngumu, au akamsamehe, atampa kivuli Mwenyezi Mungu siku ya kiyama chini ya kivuli cha Arshi yake siku ambayo hakutokuwa na kivuli ispokuwa kivuli chake.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika Mwenyezi Mungu ameandika mema na mabaya kisha akalibainisha hilo, atakayepania kufanya jema kisha akawa hakulifanya analiandika Mwenyezi Mungu kwake jema kamili, na akilipania na akalifanya analiandika Mwenyezi Mungu kwake kuwa ni mema kumi mpaka kufikia ziada ya mia saba mpaka ziada nyingi zaidi.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika Mwenyezi Mungu hatazami katika mili yenu wala katika sura zenu, lakini anaangalia katika nyoyo zenu na matendo yenu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Tukiwa sisi tumekaa kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- siku moja, ghafla akatokeza mwanaume mmoja, mwenye nguo nyeupe sana, mwenye nywele nyeusi sana, hazionekani kwake athari za safari, na wala hakuna anayemfahamu yeyote katika sisi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Mwenye kufanya ibada ambayo haipo katika dini yetu atarudishiwa mwenyewe
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Enyi waja wangu, Hakika mimi nimeharamisha dhulma katika nafsi yangu na nimeifanya kati yetu kuwa ni haramu hivyo msidhulumiane, Enyi waja wangu, nyinyi wote mmepotea ila yule niliyemuongoza niombeni uongofu nikuongozeni
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Ewe kijana, hakika mimi ninakufundisha maneno: Muhifadhi Mwenyezi Mungu atakuhifadhi, muhifadhi Mwenyezi Mungu utamkuta mbele yako, utakapoomba basi muombe Mwenyezi Mungu, na utakapotaka msaada basi taka msaada kwa Mwenyezi Mungu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Umma wangu wote utaingia peponi ispokua atakaye kataa, akaulizwa ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni nani atakaye kataa? akajibu: Mwenye kunitii ataingia peponi na mwenye kuniasi atakuwa amekataa
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni miongoni mwao
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nilimuuliza Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- Ni dhambi ipi kubwa? Akasema: Ni kumuwekea Mwenyezi Mungu mshirika, na haliyakuwa yeye ndiye aliyekuumba
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Si halali kwa muislamu kumhama ndugu yake zaidi ya siku tatu, wanakutana: huyu anampuuza huyu, na huyu anampuuza huyu, na mbora wao ni yule anayeanza kwa salamu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayemdhuru muislamu naye Mwenyezi Mungu atamdhuru, na atakayempa ugumu muislamu naye Mwenyezi Mungu atampa ugumu.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika nyinyi mtamuona Mola wenu kama mnavyouona mwezi huu, Hamtopata tabu katika kumuona kwake.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Je nikuagize katika yale aliyoniagiza kwayo Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake? Usiache picha yoyote ispokuwa umeifuta, wala kaburi lililonyanyuliwa ispokuwa umelisawazisha.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Sio miongoni mwetu mwenye kuitakidi mikosi kupitia ndege,au mwenye kuwa kuhani au akafanyiwa ukuhani,au akafanya uchawi,au akataka afanyiwe uchawi, na atakaye mwendea kuhani na akamsadikisha ayasemayo, basi huyo kayakufuru aliyokuja nayo Muhammad- Rehma na amani ziwe juu yake.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayemuendea mpiga ramli akamuuliza kuhusu lolote, akamsadikisha haitokubaliwa kwake swala yoyote siku arobaini.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayejifunza sehemu katika elimu ya nyota; basi atakuwa kajifunza sehemu katika uchawi, amezidisha anavyozidisha.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Madhambi makubwa kuliko yote: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kujiaminisha na adhabu za Mwenyezi Mungu, na kukata tamaa na rehema za Mwenyezi Mungu, Na kufa moyo katika huruma za Mwenyezi Mungu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Imani iko zaidi ya sehemu sabini au zaidi ya sehemu sitini
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Yakwamba yeye alikuwa pamoja na Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake katika baadhi ya safari zake, akatuma mjumbe asibakishe katika shingo ya mnyama chochote kinachotundikwa ispokuwa kikatwe.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Mwenye kukitegemea kitu hufungamanishwa kwacho
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayesema: Hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu, na akayapinga yanayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, ni haramu mali yake, na damu yake, na hesabu yake ni juu ya Mwenyezi Mungu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Wenye huruma huwahurumia Ar-Rahmani -Mwingi wa huruma-, wahurumieni watu wa ardhini atakuhurumieni aliyeko mbinguni.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika Malaika huteremka katika mawingu- wakalitaja jambo lililopitishwa mbinguni, basi shetani huiba kusikia, na akalisikia, kisha akaliteremsha kwa makuhani kisha wanaongopa pamoja na neno hilo uongo mia moja toka kwao wenyewe
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakuna mja yeyote atakayeshuhudia kuwa hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammdi ni mja wake kwa kusadikisha kutoka moyoni mwake ispokuwa atamharamisha Mwenyezi Mungu kuingia motoni.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Huteremka Mola wetu Aliyetakasika na kutukuka kila usiku katika mbingu ya dunia pindi inapobakia theluthi ya mwisho Anasema: Nani mwenye kuniita, nimjibu, nani mwenye kuniomba nimpe, nani mwenye kuniomba msamaha nimsamehe
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Msiswali makaburini, wala msiyakalie makaburi.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hao ni watu ambao anapokufa kwao mja mwema, au mtu mwema, wanajenga juu ya kaburi lake msikiti, na wanachora hapo mapicha, hao ni viumbe waovu mbele ya Mwenyezi Mungu.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Umejengwa uislamu kwa mambo matano
عربي Lugha ya kiingereza Kiispania
Mwenye kuona miongoni mwenu jambo baya basi alibadilishe kwa mkono wake
عربي Lugha ya kiingereza Kiispania
Atakayefanya mema katika uislamu hatoadhibiwa kwa yale aliyoyafanya zama za ujinga
عربي Lugha ya kiingereza Kiispania
Kutosheka na mambo ya wajibu.
عربي Lugha ya kiingereza Kiispania
Twahara (usafi) ni sehemu ya imani
عربي Lugha ya kiingereza Kiispania
Na hakika aliyoyaharamisha Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni sawa na aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu
عربي Lugha ya kiingereza Kiispania
Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni msije kuapa (kupitia) kwa baba zenu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
La kwanza litakalohukumiwa kati ya watu siku ya kiyama ni katika damu.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Alipita Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika makaburi mawili, Akasema: Hakika hawa wawili wanaadhibiwa, na hawadhibiwi kwa madhambi makubwa; ama mmoja wao: alikuwa hajisitiri kutokana na mkojo, na ama huyu mwingine: Alikuwa akitembea akiwafitinisha watu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Wewe pamoja na uliyempenda
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hivi nikuhadithieni hadithi kuhusu Dajali ambayo hajawahi kuhadithia Nabii yeyote watu wake! Hakika yeye ni chongo, na hakika yeye atakuja akiwa pamoja na mfano wa pepo na moto, anayoisema kuwa ni pepo huo ndio moto
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Mtu huwa katika mwenendo wa rafiki yake wa karibu, basi na aangalie mmoja wenu ni nani anayemfanya kuwa rafiki yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Fanyeni haraka kufanya matendo kuna fitina nzito kama kipande cha usiku wa giza, anaamka mtu akiwa muislamu anafika jioni akiwa kafiri, na anashinda akiwa muumini anaamka asubuhi akiwa kafiri, anauza dini yake kwa thamani ndogo ya dunia
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, Ole wao waarabu kutokana na shari iliyokaribia, imefunguliwa leo katika ngome ya Ya-ajuju na Ma-juju mfano wa hiki, na akachora duara kwa vidole vyake viwili, kidole gumba na kile kinachofuata, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Hivi tunaweza kuangamizwa hali miongoni mwetu kuna wema? Akasema: Ndiyo, pindi uchafu utakapokithiri.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Halitoacha kumfika balaa muumini wa kiume na muumini wa kike katika nafsi yake na watoto wake na mali yake mpaka akutane na Mwenyezi Mungu Mtukufu akiwa hana dhambi lolote
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Msimfanyie Mwenyezi Mungu washirika na hali nyinyi mnajua, Amesema bin Abbas katika aya hii: Washirika, ni ushirikina, uliofichikana kuliko sauti ya mkanyago wa mdudu chungu katika jiwe kubwa jeusi katika giza nene la usiku.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Msiseme: Ni matakwa ya Mwenyezi Mungu na matakwa ya fulani, lakini semeni: Ni matakwa ya Mwenyezi Mungu kisha akataka fulani
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
kuapa kwangu kwa jina la Mwenyezi Mungu kwa uongo napenda zaidi kuliko kuapa kwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu nikisema ukweli
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika mtafuata nyenendo za wale waliokuwa kabla yenu, kiwango cha unyoya wa mshale (Yaani: taratibu taratibu), hata watakapoingia katika shimo la kenge mtaingia. Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, (Unakusudia) Mayahudi na Manaswara? Akasema: Akina nani wengine (kama si hao!)
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayelingania katika uongofu, atakuwa kwake kapata malipo mfano wa malipo ya aliyemfuata, halipunguzi hilo chochote katika malipo yao, na atakayelingania katika upotofu atakuwa kwake na madhambi mfano wa madhambi ya yule aliyemfuata, halipunguzi hilo katika madhambi yao chochote
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Ni nini kinachowaogopesha hawa? wanapatwa na ulaini (wanazikubali) katika aya zilizo wazi, na wanaangamia katika aya zinazotatiza
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Mikosi ya ndege ni shirki, na hakuna yeyote miongoni mwetu ispokuwa (ana chembe ya hilo), lakini Mwenyezi Mungu huliondoa kwa kumtegemea
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nilitoka katika kundi la Bani Aamir kwenda kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- tukasema: Wewe ni bwana wetu, basi akasema Bwana ni Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nyanyua kichwa chako na sema yasikilizwe, na omba upewe, na taka utetezi utetewe
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Tahadharini na kuchupa mipaka, bila shaka kilichowaangamiza waliokuwa kabla yenu ni kuchupa mipaka
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakuna kuambukizana maradhi wala kutuhumu mikosi kwa sababu ya ndege, wala mkosi wa Bundi,na aina zingine za ndege,wala kutuhumu kuwa mwezi wa safari unamikosi, au maradhi ya tumbo yanayompata ngamia.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hauondoi uchawi ila mchawi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Si chochote mbingu saba na ardhi saba katika kiganja cha Ar-Rahmaani -Mwingi wa rehema- isipokuwa ni kama punje ya ulezi katika mkono wa mmoja wenu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Si chochote kursiy (Mahala anapoweka miguu Ar-Rahmani) katika Arshi isipokuwa ni kama bangili la chuma lililowekwa katika ardhi ya jangwa
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakuna kuambukizana maradhi, wala kutuhumu mikosi kwa sababu ya ndege, na kinachonipendeza zaidi ni kujipa matumaini. Wakasema: Ni nini matumaini? Akasema: Ni neno jema
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nikuwa yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- Alisema kuhusu maanswari (waliowapokea maswahaba waliohama kutoka Makka): Hawapendi mtu ila muumini, na hawachukii ila mnafiki, atakayewapenda Answaar na Mwenyezi Mungu atampenda, na atakayewachukia Mwenyezi Mungu atamchukia
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Fanyeni matendo na muwe na msimamo, na tambueni kuwa hatosalimika mmoja wenu kwasababu ya matendo yake, wakasema: Hata wewe Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?! Akasema: Hata mimi isipokuwa atakaponifunika mimi Mwenyezi Mungu kwa huruma zake na fadhila zake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Na hakuna Nabii aliyetumwa na Mwenyezi Mungu katika umma wowote kabla yangu, isipokuwa anakuwa katika umma wake na watu wake wapendwa na watu wanaoyachukua mafundisho yake na wanafuata amri yake, kisha wanakuja kutofautiana baada yao watu wanaowafuata, wanazungumza yale wasiyoyafanya, na wanafanya ambayo hawakuamrishwa
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nimepewa mambo matano, hajapewa yeyote katika manabii kabla yangu: nimenusuriwa (nimeepushwa) na hofu kiasi cha kutembea mwezi mzima, na imefanywa ardhi kwangu kuwa ni msikiti na ni mahala twahara (safi)
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hivi nisikuelezeni watu wa peponi? Kila mnyonge mwenye kujishusha, na lau kama angeliapia kwa Mwenyezi Mungu basi angelimuepusha na kila linalompa uzito, Hivi nisikuelezeni watu wa motoni? kila jeuri mkali mwenye kiburi.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika peponi kuna daraja mia moja kaziandaa Mwenyezi Mungu kwaajili ya wenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kati ya daraja mbili ni kama masafa ya baina ya mbingu na ardhi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Amesema Mwenyezi Mungu -Mtukufu- mimi niko katika dhana ya mja wangu kwangu, na mimi niko pamoja naye pindi anaponikumbuka
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kutoka maeneo ya Najid, kichwa chake kikiwa kimetimka, tunasikia mvumo wa sauti yake, na wala hatuelewi anasema nini, mpaka akasogea karibu kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ghafla akaanza kuuliza kuhusu uislamu.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Siku bora lililochomoza jua ndani yake ni siku ya ijumaa: Ndani yake kaumbwa Adam, na ndani yake kaingizwa peponi, na ndani yake katolewa humo
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika atakuja mtu mnene tena mkubwa siku ya kiyama akiwa halingani mbele ya Mwenyezi Mungu hata na uzito wa bawa la mbu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hato msitiri mja mja mwenzie duniani isipokuwa atamsitiri Mwenyezi Mungu siku ya kiyama
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Tulikuwa kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- watu tisa au nane au saba, akasema: Hivi hamumpi ahadi ya utiifu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayepatwa na umasikini akaushusha kwa watu hautozibwa umasikini wake, na atakayeushusha kwa Mwenyezi Mungu, basi ni karibu zaidi Mwenyezi Mungu kumpa riziki ya haraka au ya baadaye
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Muislamu atakapoulizwa kaburini anashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Hiyo ndiyo kauli yake Mtukufu: "Huwapa umakinifu Mwenyezi Mungu wale walioamani kwa kauli thabiti katika maisha ya dunia na katika akhera
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nimeamrishwa nipambane na watu mpaka washuhudie kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na wasimamishe swala, na watoe zaka, pindi watakapofanya hivyo watakuwa wamezikinga kutokana nami damu zao na mali zao isipokuwa kwa haki ya uislamu na hesabu yao itakuwa juu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika Mwenyezi Mungu ameniondolea mimi kwa umma wangu (madhambi ya) kukosea na kusahau, na yale waliyolazimishwa
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Alifariki Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- hali yakuwa hakuna chochote nyumbani kwake anachoweza kukila mwenye ini (uhai) ila kiasi kidogo cha ngano kilichokuwa katika ubao wangu (wa kuhifadhia chakula), nikala mpaka kikakaa muda mrefu, nilipokipima kikamalizika
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atasogezwa muumini siku ya kiyama kwa Mola wake mpaka aweke upande wake kwake, kisha amtake akiri makosa yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Yeyote atakaetubebea silaha, si miongoni mwetu.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa