عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيِّ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«إِنَّ اللَّهَ تَبَارَكَ وَتَعَالَى يَقُولُ لِأَهْلِ الجَنَّةِ: يَا أَهْلَ الجَنَّةِ؟ فَيَقُولُونَ: لَبَّيْكَ رَبَّنَا وَسَعْدَيْكَ، فَيَقُولُ: هَلْ رَضِيتُمْ؟ فَيَقُولُونَ: وَمَا لَنَا لاَ نَرْضَى وَقَدْ أَعْطَيْتَنَا مَا لَمْ تُعْطِ أَحَدًا مِنْ خَلْقِكَ؟ فَيَقُولُ: أَنَا أُعْطِيكُمْ أَفْضَلَ مِنْ ذَلِكَ، قَالُوا: يَا رَبِّ، وَأَيُّ شَيْءٍ أَفْضَلُ مِنْ ذَلِكَ؟ فَيَقُولُ: أُحِلُّ عَلَيْكُمْ رِضْوَانِي، فَلاَ أَسْخَطُ عَلَيْكُمْ بَعْدَهُ أَبَدًا».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 6549]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
“Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na Kutukuka, atawaambia watu wa Peponi: Enyi watu wa Peponi? Watasema: Labeka tumekuitikia na umetukuka, atasema: Je, mmeridhika? Watasema: Tuna nini mpaka tusiridhike hali yakuwa umetupa mambo ambayo hujampa yeyote katika viumbe wako? Atasema: Mimi nitakupeni kilicho bora zaidi kuliko hilo, Watasema: Ewe Mola Mlezi, ni kitu gani kilicho bora kuliko hili? Atasema: Ninawapeni radhi zangu, wala sitowachukia baada yake milele".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 6549]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia watu wa Peponi wakiwa humo: Enyi watu wa Peponi, nao watamjibu kwa kusema: Labeka, tumekuitikia Mola wetu Mlezi! na utukufu ni wako, Atasema kuwaambia: Je! mmeridhika? Watasema: Ndiyo, tumeridhika; Kwa nini tusiridhike wakati umetupa ambacho hukumpa kiumbe wako yeyote! Atasema Mtukufu: Je, nisikupeni kilicho bora kuliko hicho? Watasema: Ewe Mola Mlezi, na ni kitu gani kilicho bora kuliko hicho? Atasema: Ninakuteremshieni juu yenu radhi zangu daima; na sitokukasirikieni baada yake milele.