عَن أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنهُ عَنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«إِنَّ أَدْنَى مَقْعَدِ أَحَدِكُمْ مِنَ الْجَنَّةِ أَنْ يَقُولَ لَهُ: تَمَنَّ فَيَتَمَنَّى، وَيَتَمَنَّى، فَيَقُولُ لَهُ: هَلْ تَمَنَّيْتَ؟ فَيَقُولُ: نَعَمْ، فَيَقُولُ لَهُ: فَإِنَّ لَكَ مَا تَمَنَّيْتَ وَمِثْلَهُ مَعَهُ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 182]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira Allah amridhie kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Hakika, mwenye kiwango cha chini zaidi kati yenu katika Pepo ni kwamba ataambiwa: "Tamani!" Basi atatamani na atamani, na ataambiwa: "Je umeshatamani?" Atasema: "Nidyo." Ataambiwa: "Ni vyako vyote ulivyotamani, na mfano wake pamoja navyo."
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 182]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwenye nafasi na daraja ndogo zaidi kwa wale watakaoingia peponi, ataambiwa: Tamani, basi atatamani, na atatamani tena, mpaka atafikia mahali ataishiwa yote ya kutamani isipokuwa atayataja, hapo ataambiwa: Je, umetamani umefika mwisho? Atasema: Ndiyo, hapo ataambiwa: Basi ni vyako vyote ulivyotamani na mfano wake pamoja navyo.