عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ وَأَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنهما عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«يُنَادِي مُنَادٍ: إِنَّ لَكُمْ أَنْ تَصِحُّوا فَلَا تَسْقَمُوا أَبَدًا، وَإِنَّ لَكُمْ أَنْ تَحْيَوْا فَلَا تَمُوتُوا أَبَدًا، وَإِنَّ لَكُمْ أَنْ تَشِبُّوا فَلَا تَهْرَمُوا أَبَدًا، وَإِنَّ لَكُمْ أَنْ تَنْعَمُوا فَلَا تَبْأَسُوا أَبَدًا» فَذَلِكَ قَوْلُهُ عَزَّ وَجَلَّ: {وَنُودُوا أَنْ تِلْكُمُ الْجَنَّةُ أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ} [الأعراف: 43].
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2837]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yao- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Atanadi mwenye kunadi: "Hakika, mtapata afya nzuri na wala hamtougua milele. Na hakika, mtakuwa hai na wala hamtokufa milele, na hakika mtakuwa vijana na wala hamtazeeka milele. Na hakika, mtastareheka na wala hamtapata shida yoyote milele." Na hayo ndiyo kauli yake Mwenye Nguvu, Mtukufu: "Na wataitwa; (waambiwe) hiyo mbele yenu ndio pepo mliyorithishwa kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyafanya" [Al-Araf: 43].
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2837]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwenye kunadi atanadi kuwaita watu wa peponi wakiwa humo wakineemeka: Hakika leo hii mtapata afya na hamtaugua peponi kamwe, kwa namna yoyote ile yatakavyokuwa madogo maradhi hayo, na hakika mtapewa uhai wala hamtakufa humo milele hata usingizi pia hamtaupata ambao ndio kifo kidogo, na leo mtaishi humo mkiwa vijana na wala hamtozeeka humo milele, nakuwa mtaneemeka humo wala hamtohuzunika milele, na hiyo ni kauli yake Mtukufu: "Na wataitwa (waambiwe) hiyo mbele yenu ndio pepo mliyorithishwa kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyafanya" [Al-Araf: 43].