Orodha ya Hadithi

Hivi nisikuelezeni juu ya dhambi kubwa kuliko yote?
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Madhambi makubwa: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kuwaasi wazazi wawili na kuuwa nafsi, na kiapo cha uongo.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
"Jiepusheni na mambo saba yenye kuangamiza, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni yapi hayo? Akasema: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na uchawi, na kuuwa nafsi aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu ispokuwa kwa haki, na kula riba, na kula mali ya yatima, na kukimbia siku ya mapambano, na kuwazulia machafu wanawake waumini wenye kujihifadhi wenye kujizuia na machafu".
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Mimi nimejitosheleza na washirika juu ya kushirikishwa; atakayefanya jambo lolote akamshirikisha pamoja nami mwingine nitamuacha na shirki yake au (na mshirika wake).
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakaye shuhudia kuwa hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika nakuwa Muhammadi ni mjumbe wake na ni mja wake, nakuwa Issa ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na neno lake alilolipeleka kwa Mariam na ni roho toka kwake, na pepo ni kweli na moto ni kweli, Atamuingiza Mwenyezi Mungu peponi kulingana na yale aliyokuwa nayo katika matendo.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayekutana na Mwenyezi Mungu hali yakuwa hamshirikishi na chochote ataingia peponi, na atakaye kutananaye hali yakuwa anamshirikisha na chochote ataingia motoni.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Pepo iko karibu na mmoja wenu kuliko hata kisigino cha kiatu chake, na moto mfano huo huo.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Watakapo kutana waislamu wawili kwa mapanga yao basi muuwaji na muuliwaji wote motoni.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika halali iko wazi na hakika haramu iko wazi, na kati ya hayo kuna mambo yenye kutatiza hawayafahamu wengi katika watu, atakaye yaepuka mambo yenye kutatiza basi atakuwa ameitakasa dini yake na heshima yake, na atakayetumbukia katika mambo yenye kutatiza atakuwa katumbukia katika haramu.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika Mwenyezi Mungu hatazami katika mili yenu wala katika sura zenu, lakini anaangalia katika nyoyo zenu na matendo yenu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu hulipwa kwa lile alilolinuia
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika watu wanaovuruga katika mali ya Mwenyezi Mungu bila haki, watakuwa na adhabu ya moto siku ya kiyama.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Kila mwanadamu ni mkosefu, na mbora wa wakosefu ni wale wenye kutubia
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Sijaacha baada yangu fitina ambayo inamadhara zaidi kwa wanaume kuliko wanawake.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hawezi kuamini mmoja wenu mpaka niwe napendeka kwake zaidi kuliko mtoto wake, na mzazi wake, na watu wote.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Mwenye kukitegemea kitu hufungamanishwa kwacho
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Twahara (usafi) ni sehemu ya imani
عربي Lugha ya kiingereza Kiispania
Alipita Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika makaburi mawili, Akasema: Hakika hawa wawili wanaadhibiwa, na hawadhibiwi kwa madhambi makubwa; ama mmoja wao: alikuwa hajisitiri kutokana na mkojo, na ama huyu mwingine: Alikuwa akitembea akiwafitinisha watu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika dunia ni tamu, ni ya kijani, na hakika Mwenyezi Mungu anakumilikisheni ndani yake aone ni namna gani mtafanya, iogopeni dunia na waogopeni wanawake; kwani hakika fitina ya kwanza ya wana wa Israeli ilikuwa kwa wanawake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Wewe pamoja na uliyempenda
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika bila shaka mfano wa rafiki mwema na rafiki muovu, ni kama mfano wa mbeba miski, na mfua vyuma
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Ewe mwenye kuzigeuza nyoyo uthibitishe moyo wangu katika Dini yako.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayemuomba Mwenyezi Mungu shahada (yaani kufa shahidi) kwa ukweli, basi atamfikisha daraja ya mashahidi hata kama atafia juu ya godoro lake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Halitoacha kumfika balaa muumini wa kiume na muumini wa kike katika nafsi yake na watoto wake na mali yake mpaka akutane na Mwenyezi Mungu Mtukufu akiwa hana dhambi lolote
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Ajabu iliyoje ya jambo la muumini, hakika jambo lake lote ni kheri, na hakuna hilo kwa yeyote ila kwa muumini: akipatwa na jambo lenye kufurahisha anashukuru ikawa hilo ni kheri kwake, na akipatwa na madhara anasubiri likawa hilo ni kheri kwake.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Je nisikuelezeni kwa kile ambacho ninakiogopea zaidi kwenu nyinyi kuliko hata masihi dajali? Wakasema: Tueleze ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema: Ni shirki iliyofichikana, anasimama mtu kuswali anapendezesha swala yake kwakuwa anaona kuna mtu anamtazama
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Ee fulani, una nini wewe? kwani hukuwa unaamrisha mema na unakataza mabaya? atasema: Ndivyo, nilikuwa nikiamrisha mema na wala siyafanyi, na ninakataza mabaya na ninayafanya
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hili ni jiwe lililotupwa motoni tangu miaka sabini, anaporomoka motoni sasa hivi mpaka kaishia katika kina chake ndio maana mkasikia kishindo chake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nilikuwa kwa Saidi bin Jubair akasema: Ni nani kati yenu aliyeiona nyota iliyodondoka jana usiku? Nikasema: Mimi, kisha nikasema: Ama mimi sikuwa katika swala, lakini niling'atwa (na Nge)
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakuna kuambukizana maradhi wala kutuhumu mikosi kwa sababu ya ndege, wala mkosi wa Bundi,na aina zingine za ndege,wala kutuhumu kuwa mwezi wa safari unamikosi, au maradhi ya tumbo yanayompata ngamia.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Haitokei kuuliwa nafsi yoyote kwa dhulma isipokuwa hupata binadamu wa mwanzo fungu (la dhambi) kutoka katika damu hiyo, kwasababu yeye ndiye muanzilishi wa kwanza kuua.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Zuia ulimi wako, na ikutosheleze nyumba yako, na ulie juu ya makosa yako
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika peponi kuna daraja mia moja kaziandaa Mwenyezi Mungu kwaajili ya wenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kati ya daraja mbili ni kama masafa ya baina ya mbingu na ardhi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Laiti Dunia ingelingana na ubawa wa mbu kwa thamani yake mbele ya Allah mtukufu basi kafiri asingekunywa fundo moja la maji.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Macho ya aina mbili hautoyagusa moto: Jicho lililolia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu, na jicho lililokesha likilinda kwaajili ya Mwenyezi Mungu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika kila umma una mtihani wake, na mtihani wa umma wangu: ni mali
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Umma wangu wote watasalimika isipokuwa wenye kuyatangaza (madhambi)
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Asife mmoja wenu isipokuwa naye awe na dhana nzuri na Mwenyezi Mungu Mtukufu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Lau kama ningekuwa na dhahabu kubwa mfano wa mlima Uhudi, basi ningependa zisipite siku tatu nikiwa namiliki chochote katika mali hiyo zaidi ya kile ninachokihifadhi kwaajili ya kulipa madeni
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Si chochote dunia katika Akhera isipokuwa ni kama mfano wa mmoja wenu anapoweka kidole chake baharini, kisha atazame kimerudi na nini?
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika katika yale ninayoyahofia zaidi kwenu nyinyi baada yangu ni yale yatakayofunguliwa kwenu miongoni mwa ua la dunia na pambo lake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayetoa vitu vya namna mbili katika njia ya Mwenyezi Mungu huitwa katika milango ya pepo, ewe mja wa Mwenyezi Mungu hii ni kheri, atakayekuwa miongoni mwa watu wa swala ataitwa katika mlango wa swala, atakayekuwa katika watu wa jihadi ataitwa katika mlango wa jihadi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika mwenye adhabu nyepesi zaidi katika watu wa motoni siku ya kiyama, ni mtu atawekewa ndani ya nyayo zake makaa mawili ya moto, utakuwa ukitokota kupitia hayo ubongo wake, na yeye atakuwa akiona kuwa hakuna mtu mwenye adhabu kali zaidi yake, na hakika kumbe yeye ndiye mwenye adhabu nyepesi kuliko wao
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Yanamfuata maiti mambo matatu: familia yake na mali yake na matendo yake, vinarudi vitu viwili na kinabakia kimoja: wanarudi familia yake na mali yake, na yanabakia matendo yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa