+ -

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضيَ اللهُ عنهُ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«إِنَّ فِي الْجَنَّةِ لَسُوقًا، يَأْتُونَهَا كُلَّ جُمُعَةٍ، فَتَهُبُّ رِيحُ الشَّمَالِ فَتَحْثُو فِي وُجُوهِهِمْ وَثِيَابِهِمْ، فَيَزْدَادُونَ حُسْنًا وَجَمَالًا، فَيَرْجِعُونَ إِلَى أَهْلِيهِمْ وَقَدِ ازْدَادُوا حُسْنًا وَجَمَالًا، فَيَقُولُ لَهُمْ أَهْلُوهُمْ: وَاللهِ لَقَدِ ازْدَدْتُمْ بَعْدَنَا حُسْنًا وَجَمَالًا، فَيَقُولُونَ: وَأَنْتُمْ وَاللهِ لَقَدِ ازْدَدْتُمْ بَعْدَنَا حُسْنًا وَجَمَالًا».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2833]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake: Ya kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Hakika Peponi kuna Soko, watakuwa wakienda hapo kila siku ya Ijumaa, basi utavuma upepo wa kaskazi utawamwagikia katika nyuso zao na nguo zao, na hapo wataongezeka uzuri na urembo, watarudi kwa familia zao wakiwa wameongezeka uzuri na urembo, watasema kuwaambia: Wallahi mmezidi uzuri na urembo baada yetu, watasema: Na nyinyi Wallahi hakika mmezidi uzuri na urembo baada yetu".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2833]

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Peponi kuna sehemu watu watakuwa wakikusanyika hapo, hapatokuwa na kuuza wala kununua, bali watakuwa wakichukua kutoka hapo wanachokitaka, watakuwa wakienda hapo kwa kiasi cha siku saba, utavuma upepo wa kaskazi, utatikisa katika nyuso zao na nguo zao, wataongezeka uzuri na urembo, watarudi kwa familia zao wakiwa wameongezeka uzuri na urembo, watasema kuwambia: Wallahi hakika mmezidi uzuri na urembo baada yetu, na wao watasema: Na nyinyi Wallah hakika mmezidi uzuri na urembo baada yetu.

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumebainishwa ya kwamba watu wa Peponi watakuwa wakiongezeka uzuri na urembo.
  2. Hadithi hizi zinampelekea mtu kuwa na hamu ya kutenda mema ambayo hutumika kumfikisha mtu katika nyumba hii.
  3. Ameutaja upepo wa kaskazi pekee; kwa sababu ndio uliokuwa upepo mzuri zaidi kwa waarabu kwani ndio ulikuwa ukija na kheri na mvua.
  4. Himizo la kuwaita watu kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwahamasisha kuhusu pepo na neema zake.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kiassam الهولندية الغوجاراتية الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama