+ -

عَن أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ:
سَأَلَ رَجُلٌ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ، إِنَّا نَرْكَبُ البَحْرَ، وَنَحْمِلُ مَعَنَا القَلِيلَ مِنَ الْمَاءِ، فَإِنْ تَوَضَّأْنَا بِهِ عَطِشْنَا، أَفَنَتَوَضَّأُ مِنَ الْبَحْرِ؟ فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «هُوَ الطَّهُورُ مَاؤُهُ، الحِلُّ مَيْتَتُهُ».

[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي والنسائي وابن ماجه وأحمد] - [سنن الترمذي: 69]
المزيــد ...

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika sisi tunasafiri Baharini, na tunabeba maji kidogo sana, tukiyatumia kutawadha tunakosa maji ya kunywa, je, tunaweza kutawadha kwa maji ya Bahari? Akasema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Ni safi Maji yake na ni halali mizoga yake".

[Sahihi] - - [سنن الترمذي - 69]

Ufafanuzi

Mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Hakika sisi tunapanda majahazi Baharini kwa ajili ya uvuvi au safari za kibiashara na mfano wa hayo, na tunabeba katika safari zetu maji kidogo katika maji yanayofaa kunywa, endapo tukiyatumia maji ya kunywa kwa udhu na kuoga basi yatamalizika, na hatutoweza kupata maji ya kunywa, je, inafaa kwetu sisi tutawadhe kwa maji ya Bahari?
Akasema rehema na amani ziwe juu yake kuhusu maji ya Bahari: Maji yake ni safi na yanaweza kusafisha kitu kingine; yanafaa kutawadha na kuoga, na ni halali kula vinavyotoka humo kama samaki na nyangumi na vinginevyo hata kama vitapatikana vimekufa na vinaelea juu yake pasina kuvuliwa.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Thai German Pashto Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية النيبالية الرومانية Luqadda Oromaha
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Mizoga ya wanyama wa baharini ni halali, na makusudio ya mizoga: Ni wale wanyama wa ndani ya bahari waliokufa katika wale waliofia humo miongoni mwa wale ambao hawaishi isipokuwa ndani ya maji.
  2. Kumjibu muulizaji kwa majibu zaidi ya kile alichouliza kwa ajili ya kukamilisha faida.
  3. Maji yakibadilika ladha yake au rangi yake au harufu yake kwa kitu chochote twahara (safi) basi hayo yataendelea kubaki katika utwahara wake madam bado yako katika uhalisia wake, hata kama chumvi yake itazidi au joto lake au baridi yake na mfano wa hivyo.
  4. Maji ya Bahari yanaondoa hadathi kubwa na ndogo, (uchafu usioonekana kama janaba) na yanaondoa najisi iliyojitokeza katika kitu twahara, kama mwili, au nguo, na kinginecho.