+ -

عَن عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما قَالَ: سُئِلَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الْمَاءِ وَمَا يَنُوبُهُ مِنَ الدَّوَابِّ وَالسِّبَاعِ، فَقَالَ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«إِذَا كَانَ الْمَاءُ قُلَّتَيْنِ لَمْ يَحْمِلِ الْخَبَثَ».

[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي والنسائي وابن ماجه وأحمد] - [سنن أبي داود: 63]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdallah bin Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao amesema: Aliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu maji, na vile vinavyoyaendea kama wanyama wa kawaida na wanyama pori, akasema rehema na amani ziwe juu yake:
"Maji yatakapokuwa ni kulataini (Mapipa mawili) basi hayashiki uchafu".

[Sahihi] - - [سنن أبي داود - 63]

Ufafanuzi

Aliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu hukumu ya utwahara wa maji ambayo yanazungukiwa na wanyama wafugwao na wanyamapori kwa ajili ya kunywa na mfano wake, akasema rehema na amani ziwe juu yake kuwa: Maji yakifikia kipimo cha pipa mbili kubwa, ambazo zitakuwa na ujazo wa lita (210) basi hayo ni maji mengi hayawezi kunajisika; isipokuwa ikibadilika kwa najisi moja kati ya sifa zake tatu, rangi yake, au ladha yake au harufu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Thai Pashto Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الرومانية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Maji yananajisika ikibadilika kwa najisi moja kati ya sifa zake tatu, rangi yake, au ladha yake, au harufu yake, na hadithi imeeleza kwa ujumla na si kwa kuweka kikomo.
  2. Wamekubaliana wanachuoni kuwa maji yakibadilishwa na najisi basi yananajisika moja kwa moja, sawa sawa yawe kidogo au mengi.