عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«إِذَا اسْتَيْقَظَ أَحَدُكُمْ مِنْ مَنَامِهِ فَلْيَسْتَنْثِرْ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، فَإِنَّ الشَّيْطَانَ يَبِيتُ عَلَى خَيَاشِيمِهِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 238]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Atakapoamka mmoja wenu kutoka usingizini mwake basi na apenge kwa maji mara tatu, kwani Shetani hulala ndani ya tundu zake za pua".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 238]
Anamuhimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kuamka kutoka usingizini mwake kuwa apandishe maji puani na kuyapenga mara tatu; ambako ni kuyatoa maji puani baada ya kuyaingiza, na hii ni kwa sababu Shetani hulala ndani ya tundu za pua - nayo ni pua yote -.