عَنْ لَقِيطِ بْنِ صَبِرَةَ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ:
كُنْتُ وَافِدَ بَنِي الْمُنْتَفِقِ -أَوْ فِي وَفْدِ بَنِي الْمُنْتَفِقِ- إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: فَلَمَّا قَدِمْنَا عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَلَمْ نُصَادِفْهُ فِي مَنْزِلِهِ، وَصَادَفْنَا عَائِشَةَ أُمَّ الْمُؤْمِنِينَ، قَالَ: فَأَمَرَتْ لَنَا بِخَزِيرَةٍ، فَصُنِعَتْ لَنَا، قَالَ: وَأُتِينَا بِقِنَاعٍ -وَالْقِنَاعُ: الطَّبَقُ فِيهِ تَمْرٌ- ثُمَّ جَاءَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: «هَلْ أَصَبْتُمْ شَيْئًا؟ أَوْ أُمِرَ لَكُمْ بِشَيْءٍ؟» قَالَ: قُلْنَا: نَعَمْ، يَا رَسُولَ اللَّهِ، قَالَ: فَبَيْنَا نَحْنُ مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ جُلُوسٌ، إِذْ دَفَعَ الرَّاعِي غَنَمَهُ إِلَى الْمُرَاحِ، وَمَعَهُ سَخْلَةٌ تَيْعَرُ، فَقَالَ: «مَا وَلَّدْتَ يَا فُلَانُ؟»، قَالَ: بَهْمَةً، قَالَ: «فَاذْبَحْ لَنَا مَكَانَهَا شَاةً»، ثُمَّ قَالَ: «لَا تَحْسِبَنَّ» وَلَمْ يَقُلْ: لَا تَحْسَبَنَّ «أَنَّا مِنْ أَجْلِكَ ذَبَحْنَاهَا، لَنَا غَنَمٌ مِائَةٌ لَا نُرِيدُ أَنْ تَزِيدَ، فَإِذَا وَلَّدَ الرَّاعِي بَهْمَةً، ذَبَحْنَا مَكَانَهَا شَاةً» قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّ لِي امْرَأَةً وَإِنَّ فِي لِسَانِهَا شَيْئًا -يَعْنِي الْبَذَاءَ- قَالَ: «فَطَلِّقْهَا إِذن»، قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّ لَهَا صُحْبَةً، وَلِي مِنْهَا وَلَدٌ، قَالَ: «فَمُرْهَا» يَقُولُ: عِظْهَا، «فَإِنْ يَكُ فِيهَا خَيْرٌ فَسَتَفْعَلْ، وَلَا تَضْرِبْ ظَعِينَتَكَ كَضَرْبِكَ أُمَيَّتَكَ» فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَخْبِرْنِي عَنِ الْوُضُوءِ، قَالَ: «أَسْبِغِ الْوُضُوءَ، وَخَلِّلْ بَيْنَ الْأَصَابِعِ، وَبَالِغْ فِي الِاسْتِنْشَاقِ إِلَّا أَنْ تَكُونَ صَائِمًا».
[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي والنسائي وابن ماجه] - [سنن أبي داود: 142]
المزيــد ...
Kutoka kwa Lakitwu bin Swabira -radhi za Allah ziwe juu yake, amesema:
Nilikuwa na msafara wa bani Muntafiq -au katika msafara wa bani Muntafiq- kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, anasema: Tulipofika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hatukumkuta nyumbani kwake, na tukakutana na Aisha Mama wa Waumini, anasema: Akaamrisha tupikiwe mkate, basi tukapikiwa, anasema: Na tukaletewa Kinai -na kinai ni bakuli lenye tende- kisha akaja Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Je, mmepata chochote? Au mmeagiziwa chochote?" Anasema: Tukasema: Ndiyo, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, anasema: Wakati tukiendelea kukaa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mara tukaona mchungaji akiwaswaga mbuzi wake kuingia zizini, akiwa na kitoto cha mbuzi kikilia, akasema: "Imezaa kitoto gani ewe fulani?" Akasema: Cha kike, akasema: "Basi tuchinjie badala yake mbuzi mwingine" Kisha akasema: "Usidhanie kuwa, sisi tumemchinja mbuzi huyo kwa ajili yako, sisi tuna mbuzi mia moja hatutaki zizidi hapo, akizalisha mchungaji kitoto cha mbuzi basi tunachinja badala yake mbuzi mwingine" Anasema: Nikasema: Ewe Mjume wa Mwenyezi Mungu hakika mimi nina mwanamke katika ulimi wake kuna kitu -yaani ana maneno machafu- akasema: "Basi mpe talaka" Anasema: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika ana ujamaa na mimi na nimezaa naye watoto. Akasema: "Muamrishe" Anasema: Mpe nasaha. "Endapo atakuwa na chembe ya kheri basi atatekeleza unachomwambia, na wala usimpige mkeo kama unavyopiga mtumwa wako" Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nieleze kuhusu Udhu? Akasema: "Eneza maji ya udhu, na uachanishe kati ya vidole, na pandisha maji yafike puani, isipokuwa utakapokuwa umefunga".
[Sahihi] - - [سنن أبي داود - 142]
Ameeleza Laqitwu bin Swabira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba yeye alifika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa pamoja na watu wengine kutoka katika jamii yake ya Bani Muntafiq, anasema: Hatukumkuta nyumbani kwake, na tukamkuta Mama wa Waumini Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akaamrisha tuandaliwe mkate wa ngano na samli, na tukaletewa bakuli la tende. Kisha akaja rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Je, mmeletewa chochote katika chakula? Tukasema: Ndiyo, anasema Laqitwu: Wakati tukiwa bado tumekaa naye rehema na amani ziwe juu yake, ghafla akaja mchungaji wa mbuzi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwaswaga kwenda katika zizi lake, huku akiwa kabeba kitoto cha mbuzi kikipiga kelele, akasema: Umezalisha nini? Akasema: Jike. Akasema: Basi tuchinjie badala yake mbuzi mwingine mkubwa, kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Usidhanie kuwa sisi kwa ajili yenu tumejikalifisha na tukamchinja, bali sisi tuna mbuzi idadi yake ni mia moja, na wala hatutaki wazidi katika idadi hii, akizaliwa mbuzi mpya tunachinja badala yake mbuzi mwingine, akasema Laqitwu: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mke wangu ulimi wake ni mrefu na ana maneno machafu, nifanye nini kwake? Akasema: Basi mpe talaka. Anasema: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika nimeishi naye muda mrefu sana, na nimezaa naye. Akasema: Basi mpe nasaha, ikiwa ndani ya moyo wake kutakuwa na kheri atazifanyia kazi nasaha zako, na ikiwa hatobadilika, basi mpige kipigo kisichojeruhi, na wala usimpige kama unavyompiga mtumwa wako. Kisha akasema Laqitwu: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nieleze kuhusu Udhu. Akasema: Fikisha maji ya Udhu mahala pake, na ukipe kila kiungo haki yake, na wala usiache kitu katika faradhi zake na sunna zake, na achanisha vidole vya mikono yako na miguu yako wakati wa kuviosha, na upitilize katika kuyavuta maji ndani ya pua yako wakati wa udhu na kuyatoa kwake, isipokuwa ikiwa ulitia nia ya swaumu ili maji yasiingie tumboni mwako.