+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنهُ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«إِذَا تَوَضَّأَ الْعَبْدُ الْمُسْلِمُ -أَوِ الْمُؤْمِنُ- فَغَسَلَ وَجْهَهُ خَرَجَ مِنْ وَجْهِهِ كُلُّ خَطِيئَةٍ نَظَرَ إِلَيْهَا بِعَيْنَيْهِ مَعَ الْمَاءِ -أَوْ مَعَ آخِرِ قَطْرِ الْمَاءِ-، فَإِذَا غَسَلَ يَدَيْهِ خَرَجَ مِنْ يَدَيْهِ كُلُّ خَطِيئَةٍ كَانَ بَطَشَتْهَا يَدَاهُ مَعَ الْمَاءِ -أَوْ مَعَ آخِرِ قَطْرِ الْمَاءِ-، فَإِذَا غَسَلَ رِجْلَيْهِ خَرَجَتْ كُلُّ خَطِيئَةٍ مَشَتْهَا رِجْلَاهُ مَعَ الْمَاءِ -أَوْ مَعَ آخِرِ قَطْرِ الْمَاءِ- حَتَّى يَخْرُجَ نَقِيًّا مِنَ الذُّنُوبِ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 244]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Pindi mja muislamu au muumini atakapotawadha akaosha uso wake, madhambi yake yote yanayotokana na kuangalia yanaondoka na tone la maji au tone la mwisho usoni mwake, akiosha mikono yake yanaondoka madhambi yote yatokanayo na mikono pamoja na tone la mwisho, akiosha miguu yake madhambi yote yatokanayo na kutembea yanaondoka na tone la mwisho, mpaka muislamu anabaki msafi hana madhambi".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 244]

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakapotawadha muislamu au muumini akaosha uso wake wakati wa udhu, yanatoka katika uso wake makosa yote madogo madogo aliyoyatazama kwa macho yake pamoja na maji ya yanayodondoka baada ya kuosha, au pamoja na tone la mwisho la maji, akiosha mikono yake yanatoka katika mikono yake makosa yote madogo madogo iliyoyachuma mikono yake au pamoja na tone la mwisho la maji, na akiosha miguu yake yanatoka makosa yake yote madogo madogo iliyotembea kuyafuata miguu yake, mpaka atoke akiwa kasafishika na madhambi madogo madogo kwa kumalizika kwa udhu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Kiassam الأمهرية الهولندية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Fadhila za kuhifadhi udhu, nakuwa unafuta madhambi.
  2. Miongoni mwa muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kuwahimiza watu katika utiifu na ibada, na kutaja malipo na thawabu zake.
  3. Kila kiungo miogoni mwa viungo vya mwanadamu huingia katika baadhi ya madhambi, na ndio maana madhambi hukifuata kila kiungo kilichoyafanya, na hutoka na kila kiungo kilichotubia kwayo.
  4. Udhu una usafi wa wazi, na unakuwa pale vinapooshwa viungo vya udhu, na usafi usioonekana; na unakuwa kutokana na madhambi yaliyotokea kupitia viungo.