وعن ابن عمر رضي الله عنهما عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «أحْفُوا الشَّوَارِبَ وأَعْفُوا اللِّحَى».
[صحيح] - [متفق عليه، وهذا لفظ مسلم]
المزيــد ...

Na kutoka kwa Ibn Omar radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kutoka kwa Mtume rehema na Amani ziwe juu yake Amesema: "Punguzeni masharubu na mfuge ndevu".
Sahihi - Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim na tamko ni la Muslim

Ufafanuzi

Maana ya hadithi: Nikuwa muislamu ameamrishwa kunyoa sehemu ya masharubu yake, na asiyaache zaidi ya siku arobaini madam hajakusudia kutenda dhambi; kwa yale aliyoyapokea Muslim kutoka kwa Anas- radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- "tuliwekewa muda sisi katika kupunguza masharubu, na kupunguza makucha, na kunyofoa nywele za kwapani, na kunyoa nywele za sehemu za siri, tusiziache zaidi ya siku arobaini" na katika riwaya ya Abuudaudi: "Alituwekea sisi muda Mtume rehema na Amani zimfikie wa kunyoa nywele za sehemu za siri, na kupunguza makucha na kupunguza masharubu mara moja kwa kila siku arobaini" na imetokea kwa Ahmadi na Nasaai: "Asiye punguza masharubu yake si miongoni mwetu", Na akaisahihisha sheikh Al Baaniy katika sahihil Jaamiiy swaghiir na ziada yake (2/1113) kwa namba (6533). Hivyo kuna mkazo wa kupunguza masharubu sawasawa iwe kwa kuyanyoa mpaka weupe wa ngozi udhihiri au kwa kuyapunguza yaliyozidi juu ya mdomo ambayo yanaweza kulamba chakula. "Na kufuga ndevu" Na ndevu: wamesema watu wa lugha: ni nywele za uso na ndevu mbili maana yake ni nywele za mashavuni hizi zote ni katika ndevu. Na makusudio ya kuziachia: kuziacha zikiwa zimejaa, asijaribu kuzinyoa wala kuzipunguza, si kidogo wala nyingi; kwasababu neno kuziachia limetokana na wingi na kujazana, ziachieni na mzikithirishe, makusudio ya hilo: Nikuwa zinaachwa na zinajazwa, na zimekuja hadithi nyingi kutoka kwa Mtume rehema na Amani zimfikie zikiamrisha kuziachia, kwa matamshi mengi; zimekuja kwa neno la "Zijazeni" na kwa tamko la "Zishusheni" na kwa tamko la "fugeni". na yote hayo yanajulisha amri ya kuzibakisha na kuzijaza, na kutozifanyia ubaya. Na ilikuwa katika mazoea ya wafurusi (Wa Irani) kupunguza ndevu, sheria ikalikataza hilo, kama ilivyokuja katika Bukhariy katika hadithi za Ibn Omar "jitofautisheni na washirikina." Na amri hii pamoja na kuwekwa sababu ya kujitofautisha na washirikina inajulisha juu ya uwajibu wa kuzifuga, na asili katika kujifananisha ni haramu, na alishasema Mtume rehema na Amani zimfikie: "Atakayejifananisha na watu fulani basi na yeye ni miongoni mwao".

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Uharamu wa kunyoa ndevu au kuzipunguza, na uwajibu wa kuzifuga, tofauti na masharubu, yenyewe yanapunguzwa.
  2. Ulazima wa kuyapunguza masharubu na kutofaa kuyaacha, sawasawa iwe ni kuyapunguza kuanzia chini yake yanayokaribiana na mdomo, au kuyapunguza yote.