عن حذيفة بن اليمان رضي الله عنهما قال: «كان رسول الله صلى الله عليه وسلم إِذَا قَام من اللَّيل يُشُوصُ فَاهُ بِالسِّوَاك».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...
Kutoka kwa Hudhaifa -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoamka usiku anasafisha kinywa chake kwa mswaki.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 245]
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake mara nyingi akipiga mswaki na akiamrisha watu kufanya hivyo, na kuna baadhi ya nyakati kumetiliwa mkazo, mfano; kupiga mswaki wakati wa kuamka usiku, kwani alikuwa rehema na amani ziwe juu yake akisukutua na kutakatisha kinywa chake kwa mswaki.