عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : (لولاَ أن أَشُقَّ عَلَى أُمَّتِي؛ لَأَمَرتُهُم بِالسِّوَاك عِندَ كُلِّ صَلاَة).
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Laiti nisingeliogopea uzito kwa waumini -au kwa umma wangu-; ningeliwaamrisha kupiga mswaki kila wakati wa swala".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 252]
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake lau kama si hofu ya kuwatia tabu waumini katika umma wake basi angeliwawajibishia juu yao kutumia mswaki kwa kila swala.