عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«لَا تَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ حَتَّى تُؤْمِنُوا، وَلَا تُؤْمِنُوا حَتَّى تَحَابُّوا، أَوَلَا أَدُلُّكُمْ عَلَى شَيْءٍ إِذَا فَعَلْتُمُوهُ تَحَابَبْتُمْ؟ أَفْشُوا السَّلَامَ بَيْنَكُمْ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 54]
المزيــد ...
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -sala na amani ziwe juu yake-:
"Hamtoingia peponi mpaka muamini, na hamtoamini mpaka mpendane, je nisikufahamisheni juu ya jambo ambalo mkilifanya mtapendana? toleaneni salamu kwa wingi kati yenu".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 54]
Amebainisha Mtume Rehema na amani ziwe juu yake yakuwa hatoingia peponi ila muumini, na wala haikamiliki imani na wala haitengemai hali ya jamii ya kiislamu mpaka wapendane baina yao. Kisha akaelekeza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake katika jambo muhimu zaidi ambalo litaleta mapenzi kwa wote, nalo ni waislamu kutoleana salam baina yao, aliyoifanya Mwenyezi Mungu kuwa ni salam kwa waja wake.