عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«السَّاعِي عَلَى الأَرْمَلَةِ وَالمِسْكِينِ، كَالْمُجَاهِدِ فِي سَبِيلِ اللَّهِ، أَوِ القَائِمِ اللَّيْلَ الصَّائِمِ النَّهَارَ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 5661]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Mwenye kwenda upesi kuwasaidia wajane na maskini ni kama mwenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, au mwenye kusimama usiku na kufunga mchana"
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 5661]
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwenye kusimamia masilahi ya mwanamke aliyefiwa na mumewe na ikawa hakuna yeyote mwenye kusimamia mambo yake, na masikini muhitaji, na akawapa matumizi akitaraji malipo mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi mtu huyu katika malipo ni kama mpigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na ni kama mwenye kusimama katika swala ya tahajudi asiyechoka, na mfungaji asiyefungua.