عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم : «بَادِرُوا بالأعمال فِتَنًا كَقِطَعِ الليل المُظْلِمِ، يُصْبِحُ الرجلُ مؤمنا ويُمْسِي كافرا، ويُمْسِي مؤمنا ويُصْبِحُ كافرا، يبيعُ دينه بِعَرَضٍ من الدنيا».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Fanyeni haraka kufanya matendo kuna fitina nzito kama kipande cha usiku wa giza, anaamka mtu akiwa muislamu anafika jioni akiwa kafiri, na anashinda akiwa muumini anaamka asubuhi akiwa kafiri, anauza dini yake kwa thamani ndogo ya dunia".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Fanyeni haraka na kimbilieni katika matendo mema kabla ya kutokea kwa vikwazo, kwani zitakuja kupatikana fitina kama kipande cha giza la usiku, giza totoro, hauonekani mwangaza ndani yake, na wala hajui mtu haki iko wapi, anaamka mtu akiwa muislamu anafika jioni ni kafiri, na Mwenyezi Mungu atulinde, na anashinda muumini na anaamka kafiri, anauza dini yake kwa thamani ya dunia, sawa sawa iwe mali, au cheo, au madaraka, au wanawake, au kinginecho.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama