عَنِ الْبَرَاءِ رضي الله عنه:
عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ قَالَ فِي الْأَنْصَارِ: «لَا يُحِبُّهُمْ إِلَّا مُؤْمِنٌ، وَلَا يُبْغِضُهُمْ إِلَّا مُنَافِقٌ، مَنْ أَحَبَّهُمْ أَحَبَّهُ اللهُ وَمَنْ أَبْغَضَهُمْ أَبْغَضَهُ اللهُ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 75]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Baraa -Radhi za Allah ziwe juu yake:
Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake Alisema kuhusu maanswari (watu wa Madina): Hawampendi ila mtu muumini, na hawamchukii ila mnafiki, atakayewapenda Answaar na Mwenyezi Mungu atampenda, na atakayewachukia Mwenyezi Mungu atamchukia".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 75]
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa, kuwapenda Manswari katika watu wa Madina, ni alama ya ukamilifu wa imani; na hii ni kwa sababu ya kuwahi kwao kuutetea Uislamu na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na kuleta amani pia, na kwenda kwao mbio kuwapa hifadhi waislamu, na kutoa kwao mali zao na nafsi zao katika njia ya Mwenyezi Mungu, nakuwa kuwachukia ni alama ya unafiki. Kisha akaweka wazi -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayewapenda Manswari Mwenyezi Mungu humpenda, na atakayewachukia Mwenyezi Mungu humchukia.