عَن زَيْدِ بْنِ خَالِدٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«مَنْ جَهَّزَ غَازِيًا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَقَدْ غَزَا، وَمَنْ خَلَفَ غَازِيًا فِي سَبِيلِ اللَّهِ بِخَيْرٍ فَقَدْ غَزَا».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 2843]
المزيــد ...
Kutoka kwa Zaidi bin Khalid radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Atakaye muandaa mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu basi na yeye atakuwa kapigana, na atakayemsimamia mpiganaji kwa wema katika familia yake basi na yeye atakuwa kapigana".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 2843]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa yeyote atakayemuandalia mwenye kupigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu sababu za safari yake na anachohitaji katika silaha muhimu, vipando, chakula, gharama na vitu vingine; basi yuko katika nafasi sawa na mpiganaji, na atapata malipo ya mpiganaji.
Na atakayesimamia jambo la mpiganaji kwa wema, na akakaa badala yake katika kulea familia yake wakati asipokuwepo basi naye yuko katika hukumu ya mpiganaji.