+ -

عن ابن عباس رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
«ما مِنْ أيَّامٍ العمَلُ الصَّالِحُ فيها أحبُّ إلى اللهِ مِن هذه الأيام» يعني أيامَ العشر، قالوا: يا رسُولَ الله، ولا الجهادُ في سبيلِ الله؟ قال: «ولا الجهادُ في سبيلِ الله، إلا رجلٌ خَرَجَ بنفسِه ومالِه فلم يَرْجِعْ من ذلك بشيءٍ».

[صحيح] - [رواه البخاري وأبو داود، واللفظ له] - [سنن أبي داود: 2438]
المزيــد ...

Imepokewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao na baba yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Hakuna siku ambazo matendo mema yanapendeka zaidi ndani yake kwa Mwenyezi mungu kuliko siku hizi" Yaani: Siku kumi (za mwanzo wa Dhul-Hija), Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hata kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu? Akasema: "Hata kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, isipokuwa mtu aliyetoka kwa nafsi yake na mali yake na hakurudi na chochote katika hivyo".

[Sahihi] - - [سنن أبي داود - 2438]

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa amali njema ndani ya siku kumi za mwanzo wa mwezi Dhul-Hija ni bora kuliko siku zingine.
Masahaba -Radhi za Allah ziwe juu yao- walimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu kupigana Jihadi katika siku kumi hizi, je ni bora au kufanya matendo mema katika siku hizi? Kwakuwa linajulikana kwao kuwa Jihadi ni amali bora.
Akajibu -Rehema na amani ziwe juu yake-: Yakuwa amali njema ndani ya siku hizi ni bora kuliko Jihadi katika siku zingine, isipokuwa mtu aliyetoka Jihadi na akaihatarisha nafsi yake na mali yake katika njia ya Mwenyezi Mungu, akapoteza mali yake na ikatoka roho yake katika njia ya Mwenyezi Mungu, Hiki ndicho kilicho bora kuliko amali njema ndani ya siku hizi bora.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda kinaadiga الولوف البلغارية Luqadda Asariga الأوكرانية الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Ubora wa matendo mema katika siku kumi za Dul-Hija, ni juu ya muislamu atumie fursa ya siku hizi na azidishe ibada ndani yake, kama kumtaja Allah Mtukufu, na kusoma Qur'ani, na takbiri (Allahu Akbar) na tahlil (Laa ilaaha illa llaah) na tahmidi (Alhamdulillaah), na swala na sadaka na swaumu, na amali zote njema.