عَنِ الْبَرَاءِ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«مَا مِنْ مُسْلِمَيْنِ يَلْتَقِيَانِ فَيَتَصَافَحَانِ إِلَّا غُفِرَ لَهُمَا قَبْلَ أَنْ يَفْتَرِقَا».
[صحيح بمجموع طرقه] - [رواه أبو داود والترمذي وابن ماجه وأحمد] - [سنن أبي داود: 5212]
المزيــد ...
Kutoka kwa Barraa -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake:
"Hakuna waislamu wawili watakaokutana wakapeana mikono isipokuwa watasamehewa kabla hawajaachana".
- - [سنن أبي داود - 5212]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa hakuna waislamu wawili watakaokutana njiani na mfano wake wakasalimiana kwa kupeana mikono isipokuwa watasamehewa kabla hawajaachana kwa viwiliwili au kwa kumaliza kupeana mikono.