عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
«لَا تَجْعَلُوا بُيُوتَكُمْ قُبُورًا، وَلَا تَجْعَلُوا قَبْرِي عِيدًا، وَصَلُّوا عَلَيَّ؛ فَإِنَّ صَلَاتَكُمْ تَبْلُغُنِي حَيْثُ كُنْتُمْ».
[حسن] - [رواه أبو داود] - [سنن أبي داود: 2042]
المزيــد ...
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, na wala msilifanye kaburi langu kuwa sikukuu, na nitakieni rehema, kwani dua zenu hunifikia mahala popote muwapo".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Abuu Daud]
Anakataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- majumba kubaki tupu bila ibada ya swala ndani yake, yakawa kama makaburi ambayo hayaswaliwi ndani yake, Na akakataza kurudi mara kwa mara kutembelea kaburi lake na kukusanyika hapo kwa namna ya mazoea; kwani hilo ni njia ya kuelekea katika ushirikina, Na akaamrisha kumtakia rehema na amani juu yake mahala popote katika uso wa ardhi; kwani dua hizo humfikia kutoka kwa aliyekaribu na aliyembali kwa kiwango sawa, haina haja ya kurudi mara kwa mara katika kaburi lake.