عَنْ عَلِيٍّ رضي الله عنه قَالَ:
كُنْتُ رَجُلًا مَذَّاءً وَكُنْتُ أَسْتَحْيِي أَنْ أَسْأَلَ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِمَكَانِ ابْنَتِهِ فَأَمَرْتُ الْمِقْدَادَ بْنَ الْأَسْوَدِ فَسَأَلَهُ فَقَالَ: «يَغْسِلُ ذَكَرَهُ وَيَتَوَضَّأُ».
وَلِلبُخَاريِّ: فَقَالَ: «تَوَضَّأْ وَاغْسِلْ ذَكَرَكَ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 303]
المزيــد ...
Imepokewa Kutoka kwa Ally -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:
Nilikuwa ni mtu mwenye kutokwa na madhii kwa wingi na nilikuwa nikiona haya kumuuliza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kutokana na nafasi ya binti yake kwangu, nikamuamrisha Mikidadi bin Aswadi, akamuuliza, akasema: "Aoshe tupu yake na atawadhe" Na katika sahihi Bukhari: Akasema: "Tawadha na uoshe tupu yako".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 303]
Ameeleza Ally bin Abiy Twalib Radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa yeye ilikuwa mara nyingi akitokwa na madhii -nayo ni maji meupe mepesi yenye utelezi hutoka katika tupu wakati wa matamanio au kabla ya tendo ya ndoa-, Na wala hajui afanye nini yakitoka, akaona haya kumuuliza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake; kwa sababu yeye ni mume wa Fatma binti wa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake, Akamuomba Mikidadi bin Aswadi amuulize Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kuhuus hilo, Basi akajibu Mtume Rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa aoshe tupu yake kisha atawadhe.